MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
Nataka mtufunge ili tukichanganya na zile Hasira za Kufungwa Thalatha za Mwarabu jana tupate sababu ya Kuvurugana zaidi na Mgogoro uwe mkubwa Klabuni ili Mo Dewji ( Mwekezaji ), Salim Abdallah Mhene 'Try Again' ( Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ) na mwana Yanga SC lia lia Murtaza Mangungu ( Mwenyekiti wa Wanachama ) kwa pamoja Watuachie Timu yetu ya Simba SC kwani hawa ndiyo Wanachangia Kutuumiza mno Simba SC kwa kujifanya Wanatupenda, Wanatujali na Wanatusaidia.
Simba SC ya sasa inahitaji Vurugu, Mizozo na Fujo ili Wanafiki wote waondoke na wenye Uchungu wa kweli wa Simba SC yetu turejee rasmi Kuipambania Simba SC yetu Kimkakati na Kisayansi na kamwe si kwa Dereva wa Basi Kulazimishwa kuendesha Gari ( Basi la Timu ) Kinyumenyume kutoka Bagamoyo kwa Mganga wa Kienyeji hadi Temeke Uwanja wa Mkapa.