Ni msimu wa tano sasa Simba imekuwa ikiusubiri na hatimaye msimu huu imepata kile ilichokuwa ikikisubiri kwa muda mrefu.
Msimu wa mwisho Simba kutwaa ubingwa ilikuwa ni 2011/12.
Kwa misimu hii miwili, 2011/12 na 2017/18, ubingwa wa Simba umechangiwa mno na wachezaji kutoka Azam FC.Klabu ya Azam imekuwa ikiwatoa wachezaji hao bila kujua kuwa inatoa majembe kwa washindani wao, Simba na hatimaye kwenda kuwapa ubingwa.
1. Patrick Mafisango
Ni kiungo ambaye wanachama na mashabiki wa Simba watamkumbuka kizazi kwa kizazi.
Patrick Mafisango, kiungo Mkongomani mwenye uraia wa Rwanda, alijiunga na Simba mwaka 2011 akitokea Azam FC.
Azam ilimbadilisha mchezaji huyo na Abdulhalim Humud. Azam ilimchukua Humud kutoka Simba na kuipa Simba Mafisango.
Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zilidai kuwa viongozi walichoshwa na Mafisango kutokana na tabia yake ya utovu wa nidhamu.
Lakini hawakujua kama walikuwa wamewapa Simba jembe la maana.
Msimu huo huo wa 2011/12, Mafisango alitoa mchango mkubwa na kuisaidia Simba kutwaa ubingwa, mwenyewe akifunga mabao 11, tena mengine kwenye mechi muhimu ambazo timu ilikuwa ikihitaji ushindi kwa udi na uvumba.
Hata hivyo, hakuwa na maisha marefu ndani ya Simba kwani alifariki dunia katika ajali mbaya ya gari iliyotokea Mei 17, 2012 maeneo ya Chang'ombe Dar es Salaam.
2. John Bocco
Azam FC iliona kama vile amekwisha. Ikaachana naye, tena bila kuagana naye vizuri baada ya kuitumikia kwa muda mrefu. Akaonekana kama mzee. Hawakuona umuhimu hata wa kumuaga kwa heshima kwa kumfanyia tafrija kutokana na mchango wake mkubwa kwa kuipandisha Ligi Kuu na kucheza kwa mara ya kwanza msimu wa 2008/09.
Ni kweli hata kwa baadhi ya wachambuzi wa soka, ilionekana kama wasifu wake kisoka umemalizika. Hata alipojiunga na Simba, John Bocco alibezwa sana na watu baki, hata baadhi ya wanachama na mashabiki wa Simba.
Mabao 14 aliyofunga msimu huu akiwa Simba, yameifanya timu hiyo kutwaa ubingwa iliyokuwa ikiusaka kwa msimu mitano.
Mbali na kuifungia Simba mabao kwenye mechi ngumu, lakini pia alikuwa na mchango mkubwa kwani anapokuwapo tu uwanjani, mabeki wanaogopa kupanda, na anapokuwa hayupo pengo lake linakuwa dhahiri.
3. Shomari Kapombe
Ingawa awali alikuwa Simba, lakini alikwenda Azam FC na kuwa mmoja wa wachezaji tegemeo wa timu hiyo. Aliifanyia mengi klabu hiyo.
Hata hivyo, majeraha ya muda mrefu yaliwafanya mabosi wa Azam kuona kama angeweza kuwapisha ili wachukue damu changa.
Kapombe akasajiliwa na Simba. Haikuwa rahisi kukubalika. Alijitonesha kwenye moja kati ya mechi ya Taifa Stars dhidi ya Rwanda na majereha yake yakarejea upya.
Baadhi ya viongozi wa Simba uzalendo ukawashinda na kuona kwamba aliwatapeli tu pesa, na kwamba hakuwa na nia ya kucheza soka.
Mchezaji huyo anayecheza namba nyingi uwanjani, alianza kurejea uwanja kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar, Simba ikishinda bao 1-0. akaingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza.
4. Erasto Nyoni
Ni beki mwenye uwezo wa kucheza namba zote za nyuma, ikiwamo kiungo mkabaji. Naye aliachwa kimiujiza na Azam kwa madai tu kuwa inataka kubadilisha sera ya kutokuwa na wachezaji wenye mishahara mikubwa wala watakaosajiliwa kwa pesa nyingi.
Mkataba wake na Azam ulikuwa umemalizika. Wakati Azam ikisuasua, Yanga ilianza kumnyemelea ili kumsajili, lakini wakati ikijishauri, Simba ilimsajili kwa mkataba wa miaka miwili. Ni mmoja wa wachezaji waliotoka Azam waliochangia ubingwa wa Simba.
5. Aishi Manula
Tangu kuondoka kwa Juma Kaseja, Simba ilikuwa haijapata kipa mwenye uwezo wa hali ya juu.
Licha ya kuhangaika huku na huko hadi nje ya nchi, lakini wengi walikuwa na uwezo wa kawaida na si makipa bora kama ilivyokuwa kawaida yao, ilivyokuwa na Athumani Mambosasa, Omari Mahadhi, Idd Pazi, Mackenzie Ramadhani, Mohamed Mwameja na hatimaye Kaseja.
Hatimaye, ilipata kipa mwenye kariba hizo ambaye ni Aishi Manula.
Azam ilijibaraguza kutompa mkataba mpya kwa kigezo kile kile cha kupunguza gharama.
Hata hivyo, baada ya kelele kuwa nyingi na wachezaji karibuni wote kwenda Simba. Azam ilijirudi kutaka kumsajili Manula.
Hata hivyo, ilichelewa na Manula akajiunga na Simba. Kumaliza mechi bila kuruhusu bao ('Clean Sheat') 18 alizozipata msimu huu, zimemfanya kuwa mchezaji tegemeo aliyeipa Simba ubingwa baada ya misimu mitano, akitokea Azam FC
Nipashe