Azam fc,wamekosea wapi?

Azam fc,wamekosea wapi?

Unaujua umri wa Mazembe? Umri wa Azam? Mapema mno kuihukumu Azam? Nini maana ya MAFANIKIO kwa tafsiri yako?
Mazembe hata kabla Katumbi hajaimiliki ilishakuwa timu kubwa Azam hawatafika level ya Mazembe
 
Kuleta makocha wa Hispania ndio nia ?
Belo, acha bangi hivi kweli unaweza kuleta utitili wa benchi la ufundi wakati hunania na timu kusonga mbele...
Hispania kwasasa ndiyo wanaongoza soka hivyo naamini walileta makocha Wa nchi hiyo wakiamini watawasaidia na kumbuka vyura fc waliwahi kuleta wauza tikiti kutoka nchi moja ambayo iko vizuri kisoka wakiamini nao watachukua makombe yote ya vilabu kuanzia nchini na barani afrika...
 
Mazembe hata kabla Katumbi hajaimiliki ilishakuwa timu kubwa Azam hawatafika level ya Mazembe
Acha hizo huwezi sema eti haitakaa....mpaka sasa azam wanaenda vizuri...
 
Azam fc ilipoanzishwa nilijua itakuja kuwa kilabu bora sana afrika kama TP MAZEMBE na nyinginezo zilizofanikiwa,kwa kuwa azam fc wana boss(bakhresa) mpenda mpira na anapesa ya kutosha,nini kimewafanya wawe na uwezo kama wa simba na yanga(timu zinazoongozwa na wanachama) tu tena muda mwingine hizi timu zinaizidi azam fc(kiuwezo uwanjani).Au walichokosea ni kuingiza uyanga baada ya kumnunua mshabiki kutoka yanga(hapa natania),wamekosea wapi hawa?

Je?,unazani SIMBA na YANGA wataweza kufanikiwa zaidi ya hapo walipo wakiingia kwenye mfumo wa timu kumilikiwa na mtu mmoja au kampuni.

Wamerundika warasimu na kujifunga katika mfumo ambao hautoi nafasi mpira kuchezwa uwanjani. Club kwakuwa inauwezo wa kulipa sasa inajaza nafasi CEO, Manager mpaka humkute team coach ni hatare na anasimamiwa na watu ambao hawajawahi cheza premier Zaidi ya technical no who!

Hii ni salamu kwamba mpira unachezwa na kuongozwa na wacheza mpira, macoach na watu wa mpira waandishi wa habari hawawezi ongoza mpira hasa hawa wa bongo.

Mwenye Kampuni anania njema sema anasikiliza wapambe na undugu tofauti na vilabu vya kwengine ambapo team ni separate entity.
 
Kabla Katumbi hajainvest TP Mazembe ilishawahi kuchukua ubingwa wa Africa zaidi ya mara moja
 
Belo, acha bangi hivi kweli unaweza kuleta utitili wa benchi la ufundi wakati hunania na timu kusonga mbele...
Hispania kwasasa ndiyo wanaongoza soka hivyo naamini walileta makocha Wa nchi hiyo wakiamini watawasaidia na kumbuka vyura fc waliwahi kuleta wauza tikiti kutoka nchi moja ambayo iko vizuri kisoka wakiamini nao watachukua makombe yote ya vilabu kuanzia nchini na barani afrika...

Tatizo Azam ni Simba B na wewe unaongelea kishabiki zaidi
1.Hao makocha wa Kispaniola wamewahi kufanikiwa kwenye soka la barani Africa ? Nipe mifano
2.Tunao hao wachezaji wanaoweza kucheza soka la Kispaniola ?
3.Kocha wa Kispaniola ameletwa kuwafundisha wachezaji wazee kama Bocco,Nyoni,Agrey Morris
4.Kulikuwa na sababu ya msingi Azam kumfukuza kocha aliyewapa ubingwa Omog ambaye anafanya vizuri Simba ?

Azam licha ya wamiliki kuwa na fedha lakini inaendeshwa kiswahili kama Simba,Yanga,Ndanda na kwa sasa hakuna dalili ya wao kufanya mapinduzi yeyote kwenye soka la Tanzania.Ukipita kwenye website yao hadi sasa Stewart Hall ndio kocha mkuu akisaidiwa na Dennis Kitambi
 
Na hata Toto Africa ambayo ni Yanga B sidhani kama kuna siku watakuwa kama Tp Mazembe

Bila shaka wanalaana...!
Kwa hiyo unafanananisha uwekezaji wa wa toto african ambao hata hela ya chai ni shida na Azam ambayo wanapata kila kitu kwa wakati
 
Azam fc ilipoanzishwa nilijua itakuja kuwa kilabu bora sana afrika kama TP MAZEMBE na nyinginezo zilizofanikiwa,kwa kuwa azam fc wana boss(bakhresa) mpenda mpira na anapesa ya kutosha,nini kimewafanya wawe na uwezo kama wa simba na yanga(timu zinazoongozwa na wanachama) tu tena muda mwingine hizi timu zinaizidi azam fc(kiuwezo uwanjani).Au walichokosea ni kuingiza uyanga baada ya kumnunua mshabiki kutoka yanga(hapa natania),wamekosea wapi hawa?

Je?,unazani SIMBA na YANGA wataweza kufanikiwa zaidi ya hapo walipo wakiingia kwenye mfumo wa timu kumilikiwa na mtu mmoja au kampuni.
Hapa bongo timu ni mbili tu, tuache kujitoa ufahamu, ktk kila timu ikiwemo azam kuna simba na yanga ndani yake, so ikitokea timu yoyote itakuwa ya msimu tu haijalishi wana kiasi gani cha pesa!
 
Tatizo Azam ni Simba B na wewe unaongelea kishabiki zaidi
1.Hao makocha wa Kispaniola wamewahi kufanikiwa kwenye soka la barani Africa ? Nipe mifano
2.Tunao hao wachezaji wanaoweza kucheza soka la Kispaniola ?
3.Kocha wa Kispaniola ameletwa kuwafundisha wachezaji wazee kama Bocco,Nyoni,Agrey Morris
4.Kulikuwa na sababu ya msingi Azam kumfukuza kocha aliyewapa ubingwa Omog ambaye anafanya vizuri Simba ?

Azam licha ya wamiliki kuwa na fedha lakini inaendeshwa kiswahili kama Simba,Yanga,Ndanda na kwa sasa hakuna dalili ya wao kufanya mapinduzi yeyote kwenye soka la Tanzania.Ukipita kwenye website yao hadi sasa Stewart Hall ndio kocha mkuu akisaidiwa na Dennis Kitambi
Kweli kabsa,aisee
 
Wamerundika warasimu na kujifunga katika mfumo ambao hautoi nafasi mpira kuchezwa uwanjani. Club kwakuwa inauwezo wa kulipa sasa inajaza nafasi CEO, Manager mpaka humkute team coach ni hatare na anasimamiwa na watu ambao hawajawahi cheza premier Zaidi ya technical no who!

Hii ni salamu kwamba mpira unachezwa na kuongozwa na wacheza mpira, macoach na watu wa mpira waandishi wa habari hawawezi ongoza mpira hasa hawa wa bongo.

Mwenye Kampuni anania njema sema anasikiliza wapambe na undugu tofauti na vilabu vya kwengine ambapo team ni separate entity.
Basi kibongo bongo kutengeneza timu ni mtihani,kwa jinsi ulivoeleza hapo basi hata Mo dewj atapata shida sana katika kutengeneza timu bora,ila ingawaje huyu jamaa anaonekana yuko makini,mikakat yake inaonesha
 
MO anaweza sababu wahindi wao wanaweka Zaidi maslahi ya kibiashara mbele?
 
Back
Top Bottom