Azam FC yaachana na Kocha Mkuu Moallin pamoja na msaidizi wake

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Azam FC wameachana rasmi na kocha wao mkuu Abdihamid Moallin pamoja na msaidizi wake Omary Nasser.

"Tumefikia makubaliano kwa pande mbili na Kocha wetu, Abdihamid Moallin pamoja na msaidizi wake Omary Nasser, kuachia ngazi kama kocha mkuu, na msaidizi mtawalia".

"Hata hivyo, makocha hao wataendelea kubaki kama sehemu ya idara ya ufundi klabuni kwetu katika nafasi nyingine ambazo tutazitangaza hapo baadaye".

"Kwa sasa timu itakuwa chini ya Daniel Cadena, ambaye ni kocha wa makipa hadi tutakapotangaza kocha mpya".

" Cadena ni kocha mwenye leseni ya juu kabisa ya ukocha, UEFA Pro License".

FB_IMG_1661771501628.jpg
 
Baada ya kutoa sare ya Taifa ya Jang'ombe, Azam FC wameamua kusoma Cuba mapema.

Wameona huyu Kocha hana mechi ngumu wala rahisi kwake.
Bongo bwana...kocha anafukizwa kwenye friendly match 🤣🤣🤣🤣

Ila hapa azam wameona mbali....sasa watafute kocha wa ukweli. Kama vipi wamchukue mosimane. Hawashindwi kkumlipa million 400 kwa mwezi.

Tena uzuri last week alihojiwa na super sport akasema yeye anataka new project ambayo kama ni club basi akae chini na mmiliki wa club waweke mkakati wakuingi final ya champions league mara kadha sio unaingia mara moja then unapotea. Huyu unaona kabisa ni mtu mwenye kujua wat football is.
 
Nadhani wamekurupuka.

Ni mapema mno kumhukumu kocha. Mechi mbili ambapo ameshinda moja na kutoka suluhu hazitoshi kuamua kama kocha ni mbaya au la.

Hakuna kocha anayecheza mwenyewe! hakuna kocha anayeshinda mechi 100%
 
Bongo bwana...kocha anafukizwa kwenye friendly match [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Ila hapa azam wameona mbali....sasa watafute kocha wa ukweli. Kama vipi wamchukue mosimane. Hawashindwi kkumlipa million 400 kwa mwezi
Wameamua waachane mapema, uzito wa Kikosi cha Azam FC ulimzidi mwalimu yaani.
 
Ndugu zangu, naomba mwenye utaalam haswa anieleze, upi hasa mchango wa "kocha" mzuri kwenye ushindi wa timu? Namaanisha mchango wa kocha tutaupa asilimia (%)ngapi?

Mbona makocha wanaoonekana wazuri wanakuwa na bahati ya kuwa na kikosi bora? Pep Gudiola, Mourinho, Klopp mbona walikuwa na best squad?

Hivi ni kweli Gudiola kwa mbinu zake akipewa Ruvu shooting ya sasa anaweza kushinda NBC Premier league?
 
Kocha bora anahitaji wachezaji bora vile vile wakuendana na falsafa zake. Mpira wetu Afrika makocha wanajitahidi kuendana na tabia zetu, wanasajili viongozi kisha kocha anakuja kuhangaika na wachezaji mfano Simba na kocha wao huyu Mserbia.
 
Azam FC wameachana rasmi na kocha wao mkuu Abdihamid Moallin pamoja na msaidizi wake Omary Nasser.

"Tumefikia makubaliano kwa pande mbili na Kocha wetu, Abdihamid Moallin pamoja na msaidizi wake Omary Nasser, kuachia ngazi kama kocha mkuu, na msaidizi mtawalia".

"Hata hivyo, makocha hao wataendelea kubaki kama sehemu ya idara ya ufundi klabuni kwetu katika nafasi nyingine ambazo tutazitangaza hapo baadaye".

"Kwa sasa timu itakuwa chini ya Daniel Cadena, ambaye ni kocha wa makipa hadi tutakapotangaza kocha mpya".

" Cadena ni kocha mwenye leseni ya juu kabisa ya ukocha, UEFA Pro License".

Nililiona hili mapema
 
Ndugu zangu, naomba mwenye utaalam haswa anieleze, upi hasa mchango wa "kocha" mzuri kwenye ushindi wa timu? Namaanisha mchango wa kocha tutaupa asilimia (%)ngapi?
Mbona makocha wanaoonekana wazuri wanakuwa na bahati ya kuwa na kikosi bora? Pep Gudiola, Mourinho, Klopp mbona walikuwa na best squad?

Hivi ni kweli Gudiola kwa mbinu zake akipewa Ruvu shooting ya sasa anaweza kushinda NBC Premier league?
Hawezi , kila kocha ana mifumo yake na hiyo mifumo yake inahitaji wachezaji wenye ubora kutimiza kile anachowaelekeza.

Mfano PEP anasajili wachezaji wanaoendana na falsafa zake sio kila mchezaj anaweza ending na falsafa za mwalimu.

Me kocha bora kwangu huwa nasema Fergerson kwasababu alikua na wachezajj wakawaida tu na akabeba EPL angalia kikos cha 2013 ila PEP mpe kile kikosi kama hajamaliza nafasi ya 10 huko, ila ferg mpe hiki kikos cha PEP anabeba UEFA
 
Ndugu zangu, naomba mwenye utaalam haswa anieleze, upi hasa mchango wa "kocha" mzuri kwenye ushindi wa timu? Namaanisha mchango wa kocha tutaupa asilimia (%)ngapi?
Mbona makocha wanaoonekana wazuri wanakuwa na bahati ya kuwa na kikosi bora? Pep Gudiola, Mourinho, Klopp mbona walikuwa na best squad?

Hivi ni kweli Gudiola kwa mbinu zake akipewa Ruvu shooting ya sasa anaweza kushinda NBC Premier league?
Hapo kwenye gadiola kushinda nbc akiwa na kikosi cha Ruvu shooting ni kumuonea. Mi nadhani wacheza wana nafasi kubwa kuliko kocha.
 
Back
Top Bottom