Azam FC yajiondoa Kombe la Kagame

Azam FC yajiondoa Kombe la Kagame

Wapumzike na familia zao mpaka mwezi wa 7.
Sasa kama ni mpaka mwezi wa saba, kuna shida gani kushiriki haya mashindano ambayo pia yanaanza mwezi wa Saba kwa lengo la kujiandaa na mashindano yaliyopo mbele kama vile ligi kuu, klabu bingwa n.k? Hiyo ni sehemu ya preseason tena hauna hata haja ya kwenda nje ya nchi na unajipima nguvu na timu zingine zina hadhi ya kucheza nusu fainali klabu bingwa (TP Mazembe) hayo mashindano yamepangwa kwa wakati sahihi.

Sasa si itakuwa ni upuuzi unakata hayo mashindano halafu unaenda nje ya nchi kuomba mechi za kirafiki. Kule ulaya wanaanzishaga mashindano kama AUDI cup lengo ni kutumia kama pre season.
 
Hayo mashindano yamepangwa muda mbaya. Fikiria yanaanza kipindi ambacho wachezaji wa timu nyingi wanatoka likizo. Mfano tu Yanga wamewapa wachezaji likizo hadi tar 2/July. Swali je waingie kwenye mashindano bila mazoezi?

Timu nyingi zitapeleka vijana kwenye hayo mashindano au wachezaji wageni. Mwisho wa siku yatakosa mvuto tena. Na tena yanachezwa sambamba na michuano ya Ulaya. Nadhani wangeyaacha tar waliyopanga awali.
 
Back
Top Bottom