Azam FC yanasa saini ya mshambuliaji Bernard Arthur kutoka Liberty Professional ya Ghana

Azam FC yanasa saini ya mshambuliaji Bernard Arthur kutoka Liberty Professional ya Ghana

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
e5b1181b9f0846b6130bbcbaa3fd631f.jpg
eb09deab417346e3eab2f592030fe119.jpg
Uongozi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unayofuraha kuwajulisha kuwa imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji Bernard Arthur akitokea Liberty Professional ya Ghana.

Arthur amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na matajiri hao kutoka viunga vya Azam Complex, na zoezi zima limefanikishwa na Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohammed aliyekuwa nchini Ghana kukamilisha usajili wake.

Usajili wa Arthur 20, ni sehemu ya mapendekezo ya bechi la ufundi la timu hiyo kwenye usajili huu wa dirisha dogo, anakuja kuziba pengo la Straika mwingine kutoka Ghana, Yahaya Mohammed, aliyeondoka kwa makubaliano maalumu ya pande mbili wiki chache zilizopita.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya WAFA (Ghana) na Asec Mimosa ya Ivory Coast anaungana na washambuliaji wengine wa timu hiyo katika kukiongezea makali kikosi hicho ambao ni Mbaraka Yusuph, Waziri Junior, Yahya Zayd, Shaaban Idd pamoja na wale waliopandishwa kutoka Azam B Paul Peter na Andrea Simchimba.

Liberty Professional ni moja ya timu ya kitovu kikubwa cha kutoa mastaa wa baadaye nchini Ghana, wachezaji waliotesa barani Ulaya waliowahi kupitia hapo ni nyota wa zamani wa Chelsea, Michael Essien, Sulley Muntari (Pescara Italia) na Asamoah Gyan (Kayserispor, Uturuki).

Azam FC inamatumaini makubwa kuwa usajili wa nyota huyo utaweza kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji na kutatua tatizo la ukosefu wa mabao linaloonekana, hii ikitarajia kuendeleza mbio za kuwania taji la ligi kuu ya Vodacom Tanzania walizozianza vema hadi sasa.
 
Hii miaka 20 mmh.. nina mashaka nayo
 
Nataman tuwe na azam zaidi ya kumi ligi hii...KIFUPI NATAMAN TIMU KANDAMBILI NA MIKIA ZIPOTEE KWA MUDA NI VIRUSI
 
Ila hii midevu si miaka 20...mnapotea taratibu Kwa kutokuwa na watu wa mpira...ila nataman ushindan wenu bongo..
 
atatufaa huyo maana yahaya kazingua mwenyew ukizingatia kila kitu alikua alichotaka alipewa
 
Back
Top Bottom