Azam Federation Cup: Yanga yatupwa nje ya mashindano baada ya kutandikwa magoli 2-0 na Lipuli

Azam Federation Cup: Yanga yatupwa nje ya mashindano baada ya kutandikwa magoli 2-0 na Lipuli

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Nusu fainali ya Pili ya Azam federation inapigwa Leo majira ya saa 9 na nusu alasiri katika uwanja wa Samora mkoani Iringa wanyeji Lipuli wakicheza na Yanga huku Azam wakishangilia fainali kwa kuifunga KMC
Yanga inashuka uwanjani ikichagizwa na uongozi mpya uliochanguliwa Jana chini ya Dr. Msolla na Tayari uongozi huo umeshafiki mkoani Iringa.
Mechi itaanza saa 9:30 kutoa nafasi Kama mechi hiyo itaisha sare kwenda kwenye dakika 30 za nyongeza ikishindikana Ni mikwaju ya penati
Kikosi Cha Yanga kinachoanza

======


IRINGA
TIMU ya Lipuli FC ya Iringa imefanikiwa kuingia fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarudu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya vigogo, Yanga SC Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Sasa Lipuli FC itamenyana na Azam FC katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo itakayofanyika Uwanja wa Ilulu mjini Lindi mapema mwezi ujao.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Shomary Lawi wa Kigoma, mabao ya Lipuli FC yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Paul Nonga dakika ya 27 na Daruwesh Saliboko dakika ya 38.


Wazi Yanga haitashiriki michuano ya Afrika mwakani baada ya kipigo cha leo, kwani kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara ubingwa umekaa vizuri zaidi kwa watani waol Simba SC.

Na kipigo hiki kinakuja siku moja baada ya kuchaguliwa kwa uongozi mpya wa klabu chini ya Mwenyekiti, Dk. Mshindo Mbette Msolla, Makamu Mwenyekiti Frederick Mwakalebela na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Hamad Islam 1,206, Mhandisi Bahati Faison Mwaseba 1,174, Dominick Ikute, Kamugisha Kalokola, Arafat Haji, Salum Ruvila, Saad Khimji na Rodgers Gumbo.

Uchaguzi huu umefuatia kujiuzulu kwa viongozi wote waliongia madarakani Juni 11 mwaka 2016.
Inst-image-20.jpeg
59350635_2817375138305001_2730743367892729856_n.jpeg
 
Nipo Swahiba. Mambo niaje?

Nimeguna unavyotuchawia tu Swahiba. Maana mapema yote hii tayari ushajiandaa na Updates. Lol
Me mzima
Tatizo hamchelewi kujisahalidha nimewakumbusha mapema
 
Lipuli Lindeni Heshima Yenu, Kuna Mtu Kaja Huko Jana na Mzigo wa Maana tu.
Bora Mlaumiwe Kuliko Kufedheheshwa.
Tutawaangalia Mnavyo Cheza.
 
Back
Top Bottom