Azam Group wawanyang'anya IPP wafanyakazi wa kumwaga

Rehema Salim kaondoka ITV mwishoni mwa mwezi uliopita, na amejiunga na Azam TV mwanzoni mwa mwezi huu, wala sio kitambo.
Ova
Rehema Salim au kaenda nyumbani? Maana ubini wake kama vile una uhusiano wa damu na AZM.
 

Hao azam group wakianzisha benki ya kiislam inayotoa mikopo bila riba hapo ndio nita waona wa maana.
 
siku wakimchukua GODWIN GONDWE nitaumwa kwa kweli,nampenda sana akiwa anatangaza taarifa ya habari ITV
 
EFM nayo imevuna ITV kina Abubakary Lyongo na mwenzake na sasa wanataka kuhamia Clouds Fm wanamtaka Millard Ayo, wao wanatoa mshahara mnono nyumba na gari.

Hiyo jeuri ya kufanya yote hayo wanaitoa wapi? Mi pia siamini kama kuna mtu anaweza kutoka Cloudz kwa ajili ya EFM, Labda awe na matatizo yake binafsi
 
Hao azam group wakianzisha benki ya kiislam inayotoa mikopo bila riba hapo ndio nita waona wa maana.

Mbona ipo kwenye pipeline! Unajua Azam kajipanga! Atakamata uchumi wa nchi kadri siku zinavokwenda!
Simpendi na iman yake lakini kazi anapiga!
 
Mbona ipo kwenye pipeline! Unajua Azam kajipanga! Atakamata uchumi wa nchi kadri siku zinavokwenda!
Simpendi na iman yake lakini kazi anapiga!

Ikishakua tayari mkui tujuzane tukachukue mahela japo mi sio wa imani yake hope nitakua na vigezo.
 
Dah, hadi patrick?! Mengi hebu jibu mapigo.
 
kama ni data tu mnazo jaman. mbona mnafaa kuwa wahabari zaidi ya kina patricj
 
Naomba kuuliza Fatna Ramole, na Anna Mbajo wako TV gani? Wale mbinti ni wazuri aisee, wanafaa kwa matangazo.
 
Godwin Gondwe alikataa kuajiliwa ITV anafanya kazi kwa mkataba tu.

Mbona ITV hakuna waajiriwa pale!
Mikataba yenyewe wengi tu unawaona wamevaa makoti mazuri yanaishia vifuani lakini hawana, yaani wanafanya kazi kama ma-day worker wanaopiga debe Ubungo-M/Mmoja.
Siku akifa ndio mnabaki midomo wazi, yaani mtu alikuwa na jina kubwa, kumbe hata mkataba hana.
Unamkumbuka marehemu Rehema Mwakangale?
 
Namkumbuka Rehema Mwakangale,kwani hakuwa muajiriwa wa ITV?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…