Azam hawakufanya utafiti kabla ya kumfukuza kocha

Azam hawakufanya utafiti kabla ya kumfukuza kocha

Kocha aliyefukuzwa ndiye huyohuyo ambae aliiwezesha Azam kuongoza ligi kabla ya mechi na Yanga.

Yanga walifukuza kocha lakini matokeo yamebaki yaleyale ya ushindi mwembamba kila mechi. Mtibwa, Ihefu, Namungo, KMC, Mbeya City wamebadilisha mabenchi ya ufundi lakini matokeo kwenye club yamebakia yaleyale.

Nadhani shida sio makocha bali iko kwenye:

1. Ubora wa wachezaji wa timu. Wacheza wa Azam wana uwezo unaokaribiana na wale wa timu nyingine kwenye ligi.
2. Ubora wa timu nyingine, kila timu imesajili vizuri hivyo hakuna timu mbovu kabisa.
3. Maamuzi ya marefa. Marefa wetu sio wa kiwango cha juu pia hatuna assistant referee technology.
4. Viwanja vyetu baadhi sio vizuri.
5. Makocha wetu sio wale wa level ya EPL, uwezo wao unafananafanana.
6. Uongozi wa vilabu vyetu hawana taaluma ya kuongoza soka, wanabahatisha tu.
7. Matibabu ya wachezaji wanaoumia sio ya kiwango.
8. Kuna wachezaji ambao wanacheza kila mechi, hivyo wanachoka sana.

Hivyo kumfukuza kocha kunaweza kusilete tofauti kubwa inayokusudiwa.

Msameheni
Katika mazingira hayo hayo anatakiwa ashinde
 
Kama hawajalizika watamfukuza tena, kwasabu timu inaweza kufungwa wakati ikicheza mpira wa kiburudani. Kule Zanzibar huwa wanasema kufungwa tunafungwa lakini chenga tunawala. Inamaana mpira ni furaha pia uwanjani
 
6. Uongozi wa vilabu vyetu hawana taaluma ya kuongoza soka, wanabahatisha tu.

Mimi sio mtaalam wa mpira lkn kwa uzoefu wangu kwny namba 6-uongozi hapa ndo tunafeli sana sio kwny mpira tu, hata kwny taasisi nyingine ziwe za kidini, serikali au binafsi. Kwny uongozi thabiti matatizo mengi yanaweza kudhibitiwa. Naamini tatizo la Azam ni uongozi kwa sasa, azam ni timu ilikuja vzr kiasi tukaamini itazipita Simba na Yanga kwa margin kubwa lkn mpaka sasa inaonekana ni timu ya kawaida sana with all the investment achieved so far. Nadhan kwa busara tu uongozi wa sasa uachia madaraka waje wengine na mawazo mapya.
 
Huo ndio ukweli, hata Azam media inakwenda vizuri kutokana na kuwa na viongozi kama akina Tido Mhando, Charles Hilary wenye utaalamu mkubwa wa uongozi wa media.

Kama Tido angeendelea kubaki TBC huenda ingeonyesha ligi zote za Tanzania, ngumi, CECAFA, CAF na EPL. Lakini tangu aondoke TBC kila mtu anafahamu kilichotokea TBC
 
Back
Top Bottom