AZAM: Klabu kubwa ila timu ni ya kawaida sana

Hivi hamuoni aibu kuisema Azam na kuziacha Simba na Yanga??
Hao Simba na Yanga ni sawa na Bondia sugu kila akipigwa bado anataka Mechi ya marudiano, Miaka Nenda miaka rudi hata Kiwanja cha Mazoezi wameshindwa kujenga hivyo hao si Watu wa kuigwa na Azam.
Aidha kwa uwekezaji wa Azam tulitarajia ile timu itakuwa si ya kushindanishwa na Simba au Yanga, ingepaswa kutoa Ushindani kwa Timu zinazofanya vizuri kama TP Mazembe, etc!
Au wewe unataka tuishindanishe na hao akina Singida United?
 
Nimecheka sana na nimefurahi sana yanga walivyotimuliwa asubuhi wakagomewa kufanya mazoezi shamba la bibi! Ama kweli hii ndo dawa ya timu kongwe ili waanze kufanya mikakati ya kutafuta viwanja vyao!
 
Hivi hamuoni aibu kuisema Azam na kuziacha Simba na Yanga??
Sio aibu mkuu kuisema Azam. Simba na Yanga ni timu zilizo zoeleka na Azam wengi tuliona ni mbadala wa hizo klabu kongwe hapa nchini.
 
Sawia mkuu. Azam inakuwa kama Asenali tu sasa ya England.
 
Yani mashabiki wa Yanga bhana..

Kisa Simba kaipiga Azam basi ndyo timu mbovu..

Sio timu mbovu mkuu, uwezo wa Ndemla,Okwi Na Kwasi Ni Mkubwa Mno..
Uwezo wenye wa kigoli kimoja tena kwa msaada mkubwa wa refa
 
Hujaona mafanikio ya azam.uwanja ,gari malipo mazuri yaani kipindi kifupi hatua waliyofikia naona kama tatizo kumbuka hizo TP mazembe mafanikio yao cii ya miaka 10 wamekaa mda mrefu kufikia hayo mafanikio
 
Hujaona mafanikio ya azam.uwanja ,gari malipo mazuri yaani kipindi kifupi hatua waliyofikia naona kama tatizo kumbuka hizo TP mazembe mafanikio yao cii ya miaka 10 wamekaa mda mrefu kufikia hayo mafanikio
Mkuu hiyo ilikuwa ni baadhi ya Miundombinu ya Msingi iliyokuwa kwenye Mipango ya Club toka inaanzishwa.
Hivyo uwekezaji huo ndio ungetumika kama Nyenzo ya kufanikisha Club ya Azam kufikia Mafanikio ambayo waliyatarajia au unadhani hayo ndo yalikuwa Malengo ya kuanzisha kwa Club ya Azam?
Aidha Mafanikio yanachangiwa na mambo mengi ila kubwa ni uwekezaji, Hata ukiichukuwa Mbao Leo ukaipa uwekezaji wa kutosha lazima wapate Mafanikio tu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…