Azam Kuidhamini Ligi kuu ya Uganda

Azam Kuidhamini Ligi kuu ya Uganda

dav22

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
1,887
Reaction score
312
Azam Media LTD wameingia ubia na shirikisho la soka Uganda kuidhamini ligi kuu ya nchi hiyo ambayo itakuwa ikiitwa Azam Premier League kwa kitita cha USD 1.9 leo

Na wamesema wapo katika mchakato kuomba kibali kuonyesha ligi za Uingereza,Ufaransa na Spain
 
Attachments

  • 1422875929207.jpg
    1422875929207.jpg
    54.5 KB · Views: 433
  • 1422875948044.jpg
    1422875948044.jpg
    56.5 KB · Views: 385
Dah....Hongera Sana Sana.
 
Hiyo ni habari njema sana.. Hongereni Azam kwa hilo.. Panueni wigo muikamate East Africa yote.. Mnaweza..
 
Aisee jamaa spidi yao kali sana wataikamata africa muda si mrefu
 
Hongera azam na bakhresa

Ila wengine wenye pesa za madafu kila siku kelele na viongoz wa serikali
 
Azam Media LTD wameingia ubia na shirikisho la soka Uganda kuidhamini ligi kuu ya nchi hiyo ambayo itakuwa ikiitwa Azam Premier League kwa kitita cha USD 1.9 leo

Na wamesema wapo katika mchakato kuomba kibali kuonyesha ligi za Uingereza,Ufaransa na Spain

dola ngapi?????????? Are u kidding?
 
Azam Media LTD wameingia ubia na shirikisho la soka Uganda kuidhamini ligi kuu ya nchi hiyo ambayo itakuwa ikiitwa Azam Premier League kwa kitita cha USD 1.9 leo

Na wamesema wapo katika mchakato kuomba kibali kuonyesha ligi za Uingereza,Ufaransa na Spain
Naamin hapo kwenye red utakuwa umeacha kitu kama mil. au bil. zaidi ya hapo hongera zao...wakianza kuonyesha ligi za nje hasa uingereza na mimi ntahamia azam ..
 
Azam imeingia makubaliano ya kusaini mkataba kati ya Azam Media na FUFA juu ya haki miliki za ligi kuu ya Uganda ambayo azamTV imedhamini ligi hiyo itakayotambulika sasa kama Azam Premier League.

Azam Media imeingia mkataba wenye thamani ya Dola za kimarekani zipatazo Milioni mbili sawa na fedha za kitanzania Bilioni 5.5.

Timu shiriki 16 zitapata mgao wa Milioni 60 kwa mwaka, fedha ambazo zitazisaidia vilabu hivyo kujiendeleza zaidi na kumudu gharama za uendeshaji.

Historia mpya katika ramani ya mpira wa miguu imeandikwa Uganda leo, na ni matarajio yetu kuleta mabadiliko makubwa kama tufanyavyo Tanzania na VPL.

Chanzo: Ukurasa wa Facebook wa Azam TV

attachment.php
 
Attachments

  • azam.png
    azam.png
    115.9 KB · Views: 888
Hongera sana Azam tv kwa kupiga hatua kubwa.
 
Ina maana huo udhamini ni wa Tv rights ikiweno kurusha live mechi zake? Au ni kama vodacom na ligi yetu ya bongo? Ufafanuzi tafadhali wadau
 
Back
Top Bottom