The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
Azam yeye boti yake haina hiyo Humphree system kwa ajili ya stability ni Zanzibar 1 pekee ndio ina hiyo teknolojia kwa hizo boti.
Azam K7 inatumia engine za Cummins hizi engine zina kelele sana ukilinganisha na Zanzibar 1 ambayo inatumia MTU engine.
Cummins engine zinapewa sana promo kwakuwa ni mmarekani na ni za kawaida sana, tena akikimbia mpaka knot 33 ndani ya lisaa atalazimika kutumia mafuta mengi sana.
Na kwenye speed Zanzibar 1 kama kweli ikiwekwa Full Head hiyo K7 haimpati ingawa KW(HP) kubwa kuliko Zanzibar 1.
Kilimanjaro zina stabilizer system sema sio za kisasa kama zilivyo Zanzibar 1.
Boat ambazo hazikua nazo ni Kilimanjaro 1 & 2, zile alizoziuza. Kilimanjaro 3 na 4 ziliwekewa huku tayari zikiwa zipo kazini. 5, 6 na 7 zimewekewa tokea kiwandani ila ni kutuliza boat wakati wa mawimbi. Lakini haya maelezo ni kwa mujib wa Chief Engineer Victor.
Ila kusema kweli ukipanda Zanzibar 1 kitu kimetulia kama ndege, ukichanganya na injini kuwa jet ndio kabisaaa full tambarare.