Azam mchukueni Matola kwa gharama yoyote ile mtakuja kunishukuru mbeleni

KENGE 01

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
1,705
Reaction score
4,217
USHAURI:

Kwa mabosi na wadau wa hapo Chamazi akina Saidi, Omary, Hashimu Ibwe, Zakaria (ZakaZakazi) na wengineo mnataka kujua umafia na kufanya mageuzi kwenye timu yenu basi msajili kocha mzawa kwa gharama yoyote ile Ramadhani Matola na mpeni mkataba wa miaka mi 4+.

Matola anajua umafia wa ligi hii, kaicheza ligi kwa miaka kadhaa na amekuwa kocha kwa miaka mingi.

Najua watakuja kusema hana vigezo na mambo ya leseni ya CAF, ukweli ni kwamba hayo ni mambo madogo sana ila kama mtaamua kusajili kocha Mzungu basi hamna rangi mtaacha kuiona. Msimu huu mmebadili Makocha zaidi ya wanne, ndani ya misimu miwili tu!

Nawasilisha.
Kenge1
 
'Hamna Rangi Mtaacha Kuona'.

Onyo hili Linaenda Azam...Wasipomchukua Matola.

yetu Macho na masikio.
 
Naunga mkono hoja, tunapenda sana makocha wa kigeni lakini wengi hamna kitu, mfano Zolan
 
Kwa nini awe matola na usiseme Ally Mayay Tembele.
 
Kwa nini awe matola,na usiseme ally mayay tembele.
Luh!
Ally mwajiriwa wa serikali kwenye nafasi kubwa anaweza kuacha kazi yake kweli aje Ku risk Azam?

Akifukuzwa anaenda wapi?
 
Tatizo kubwa la Azam ni viongozi sio kocha, Mimi nadhani mpaka leo sijui ya malengo ya team ya Azam ni nini?

Je wanaondoka katika ile system yao ya kuwa na team za vijana na kuwaendeleza mwisho wa siku kuja kuchezea team A au siku hizi wamegeuka Yanga na Simba ndogo?

Kama philosophy yao bado vijana ni lazima walete kocha mwenye history ya kuendeleza vijana kuwa Asset ila kama huko wamehama wanataka mafanikio ya haraka basi reqruitment yao iwe ya viwango maana pesa sio shida kwao ni nani huyu analeta wachezaji kwa pesa nyingi ila viwango vya kawaida kufungwa na KMC?

viongozi wako kula pesa ya tajiri hawako serious kuifanya Azam team ya ushindani.

Azam leo walitakiwa kuwa pace maker kuwafanya hawa wakubwa kuongeza juhudi kuleta chachu na kuongeza fan base hasa watoto ili kesho wawe na washabiki halisi.

Leo hii kuna watu Man city sababu wameanza kuona mpira wakati city mafanikio lakini huwezi kukuta watu wa 70 wanaipenda city utakuta Liver, Man u huko. wao wanataka kugombania mashabiki maslahi wa kuwalipa washangilie fursa jenga team yenye kuvutia watu wanaona mipira kwenye TV watoto wanapenda team yenye kushinda baada ya miaka watajenga fan base yao.
 
AZAM waanzishe timu za walemavu na kina dada, labda huko watatoboa, ingawa huko kwa akina dada siyo kurahisi vilevile maana Simba na wenyewe wameshawekeza nguvukazi.

AZAM ni uthibitisho kuwa pesa si suluhisho la kila kitu.
 
Ameshapata leseni A ya CAF?
 
Makocha Wazawa yupo Salum Mayanga yuko Vizuri, Yupo Minziro anatisha yupo, Matola, Amri Said na Kally Ongala wawaaamini watawavusha.
 
Team apewe mzawa ila wazungu wanajiona sana
 
Kwa nini awe matola na usiseme Ally Mayay Tembele.
Yaani Ally aache kazi aje kifindisha vichaa ambao mda wowote wakimchoka wanamtimua?itakua akili au matope
 
Matola ni kocha sana ..

Sema tu yuko ktk kivuli cha wengine kila wakati
 
Simba sidhan kama watamuachia kirahisi Matola,nahisi wana malengo nae yule.....hata kama watamuachia basi itakuwa kwa masharti magumu sana au masharti ya "Nenda urudi" masharti ambayo kimsingi yatawanufaisha simba sc.....Simba wana akili wale sio watoto.
 
Ndoivo lazima apewe ilo sharti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…