Azam Media aibu tupu. Watangazaji wake lugha ya Kiingereza ni sifuri, wanatia aibu Taifa la Tanzania

Kutojua lugha ya kiingereza si tatizo.....ila kwa kutojua kwao wanashindwa kuuliza maswali ya maana
 
Aibu gan sasa wakat sio lugha yetu yaan pale bbc mtangazaji ashindwe kuongea kiswahili au aongee kishwahili kibovu waanze kumsema kua anatia aibu taifa kwa kuongea kiswahili kibovu stukeni acheni kujishusha
 
Nakukatalia kwa Ushahidi Kuntu (Tukuka) .
Bro umeenda mbali sana ku prove ujinga na ulimbukeni wa huyu jamaa. Tumuulize tu kingereza kinatusaidia nini huku mtaani sisi waafrika ? Ukoloni bado umejaa vichwani.
Imagine mtu anasomea madini na ataenda kufanya kazi na wajita na wasukuma ila anakazania eti ajue kingereza kuliko hata kuyajua madini yenyewe na watu wanaozunguka hayo madini.
Hizo TV zipo kwa ajili ya kuwatangazia wazungu au sisi watanzania ? Isitoshe lugha yoyote kama huiongei mara kwa mara unapoteza fluency.
Mimi sioni mantiki ya watangazaji wa local TV kuwa mahiri wa kingereza badala ya kiswahili, kazi yao ni kutufikishia ujumbe sisi watanzania sio wazungu.
Huku mikoani unaweza ishi hata miaka 10 usikutane au kusikia mtu anaongea ki gereza, sasa hao waaandishi kingereza cha umahiri cha nini zaidi ya wao kuhoji tu wazungu au watu wa nje.
Je hao watu wa nje wanawahoji mara ngapi kwa mwaka, utakuta hapati client wa kumuhoji hata miaka.
TUAMKENI JAMANI TUPO KWENYE USINGIZI WA ULIMBUKENI USIO NA FAIDA.
AFRIKA HAIITAJI KINGEREZA KUENDELEA BALI MAARIFA YA VITENDO.
 
Kutojua lugha ya kiingereza si tatizo.....ila kwa kutojua kwao wanashindwa kuuliza maswali ya maana
Hayo maswali wanamuuliza nani na kwa lengo gani ? Mzungu akiulizwa swali inatusaidia nini sisi wakulima wa miti njombe ?
 
Tatizo ni kuingiza upendeleo mahali ulipaswa kuajiri mtaalamu wa lugha unaajiri shemeji yako.
 
Hata hao makocha English pia inawapa tabu wanaungaunga tu muhimu waeleweke, wewe sikiliza yale madash wewe jazia utaelewa. English sio lugha yetu, juzi sio umemuona Yamal kaulizwa kwa kizungu na Pogba bahati mbaya kile kidubwasha cha kutafsiria kikawa na shida akasema tu sijaelewa swali sababu English hajui wala sio aibu, watu wanajivunia lugha zao. Jibu kwako kutojuwa kizungu sio aibu kikubwa kazi yako unaijuwa. Yamal hajui English lakini uwanjani utajuwa shughuli yake. Messi miaka yote kabeba makombe huwezi kukuta hata clip moja anaongea English, hata kama anajuwa anajifanya hajui.
 
Kazi za kubwabwaja kwenye media hazihitaji ujue kiingereza.
 

Kujua lugha hakuna uhusiano na Shule...

Wengi unaoona wanajua lugha sana halafu ni wasomi means wamekulia mazingira ya lugha either exposure au english medium na wala si vidato.

Nenda nairobi kutana na omba omba machokoraa wanatema ngeli ya hatari.
 
Nafikiri watangazaji ni kioo tuu kuakisi uhalisia wa watanzania wengi nikimaanisha namna walivyo ndivyo tulivyo.
Bila kuathiri kukua Kwa kiswahili serikali yetu imeshindwa kutoa Elimu ya kutufanya tuwe fluently?
 
Kwanini hao makocha wasijifunze kiswahili,si wanataka matumbo yao yashibe........tunawapa kazi ngumu vijana wetu,

Tupende lugha yetu......hawa makocha wakienda kule China au Korea huwa wanahojiwa kwa lugha gani?
 
Sio hao tu, tasnia nzima ya media, journalists, ni zero tupu, sio kwa, kimombo, hata upeo wa geopolitics issues, wasafi media, zembwela na kundi lake, huongelea ngono, kufumaniana, kuanzia asubuh saa 11!
Efm ni mamipira tu, mwanzo mwisho, TBC, ndio kabisa, hata kiswhili fasaha, kinawagonga, kuna ule usemi, swaga ya kizungu, mtu ukiwa unaongea kizungu, ukasema "i will do that, and that will not be there, yo know! Sasa mbongo, utasikia, " Sikuelewi ujue! Akitafsiri kizungu, "I don't understand, you know!
Upuuzi, mtupu,Kenya, vyombo vyote via kimatsifa, nafasi za Africa, wameshika wao, BBC Africa, CNN, Reuters, nk, ukimtoa Tido muhando, Charles Hillary, nani anamfikia Jeff koinage, Ivan Mwaula, Hussein Mohamed(sasa yupo ikulu), au chombo gani cha habari kinafikia hata asilimia mbili tu ya citizen, KTN, za, Kenya!
 
Eti mulikuwa mkufunzi sehemu fulani labda mkufunzi wa lugha ya matusi
 
Tatizo ni lugha au komfidensi ya kuongea ndio hawana ? Mfano utaskia anasema hivi hii hello coach congratulations for the game πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Alitakiwa asemaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…