Tipstipstor
JF-Expert Member
- Nov 29, 2021
- 1,528
- 3,352
Nawapongeza kampuni ya Azam media kwa kuonesha mechi za ligi kuu NBC live, kitendo ambacho kimeipa hadhi ligi yetu si tu Africa ya mashariki bali Africa nzima.
Wito wangu kwa wamiliki wa Azam media ni kuwa ongezeni idadi ya Camera katika production team yenu ili muweze kunasa matukio takribani yote uwanjani.Ligi ya EPL ni bora ulimwenguni kutokana na production quality yao, wanatumia zaidi ya camera 30 uwanjani kunasa matukio yote ndani ya uwanja , pembezoni na pia kwa mashabiki jukwaani ila huku kwetu kamera zinazotumika hazizidi 3. Kamera moja tu ya jukwaa kuu ndio inatumika kunasa zaidi ya asilimia 80 ya matukio yote ndani ya uwanja.
Kitendo ambacho kinapelekea baadhi ya matukio muhimu kushindwa kuoneshwa kwa wakati mfano replays za offside kwenu zimekuwa tatizo, inaweza kutokea mchezaji kampiga mwenzake kiwiko wakati hana mpira na bado mkashindwa kuonesha tukio. Juzi wachezaji wa mbeya kwanza walileta fujo baada ya simba kupata goli na bado mlishindwa kunasa tukio, kuna kipindi wachezaji wanacheza tackiling mbaya zinazoweza kuhatarisha maisha ya soka ya mchezaji mwenzake ila mmekuwa hamnasi matukio kutokana na idadi ndogo ya camera mlizonazo.
Yusuph,Abubakar,Omar na mzee wenu bakhresa nawashauri muwapeleke uingereza,spain au ujerumani baadhi ya wafanyakazi wenu wa Azam media waende kujifunza mambo muhimu katika production. Bado mpo local sana.
Mwisho katika watangazaji wa mechi, jaribuni kuongeza mchambuzi wa mechi ili aweze kutafsiri baadhi ya sheria na matukio yanayotokea uwanjani. Watangazaji wenu kama Baraka mpenja, Hashim Ibwe, Iddi salum kidedea wanajua kuhype mechi ila sio wachambuzi wa mpira. Igeni mfano wa TBC walivyokuwa wakitumia combination ya Jesse John na Hayati Mwalim kashasha. Jesse anatangaza ili ikifika sehemu inayohitaji technical explaination anamwachia mwalim kashasha afafanue.
Ni hayo tu kwa leo.