Azam Media yanunua haki za matangazo Ligi Kuu Kenya

Azam Media yanunua haki za matangazo Ligi Kuu Kenya

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,063
Reaction score
12,866

Baada ya kuzinunua ligi kuu za Tanzania Bara (VPL) na Uganda (UPL), Kampuni ya Azam Media, leo imenunua rasmi haki za matangazo ya televisheni ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKL Premier League).

Imetangazwa rasmi leo kuwa Azam TV inayorusha matangazo kwa satelaiti kutoka Tanzania, itakuwa inarusha moja kwa moja 'live' matangazo ya mechi za ligi ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF)baada ya pande zote mbili kusaini makubaliano hayo kwenye Hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi, Kenya leo Ijumaa 20 Machi.

Udhamini huo wa miaka mitatu utazifanya mechi za FKF PL zionekana moja kwa moja kwa dau la dola za Marekani (US$ 2.25milioni sawa na Kshs 204,750,000) ikiwa ni sawa na US$ 750,000 kwa kila msimu.

Imethibitisha na Mwenyekiti wa FKF, Sam Nyamweya, kwamba kila timu inayoshiriki ligi hiyo itapata fungu la Kshs 1milioni kila mwezi huku akitamba kuwa misaada mingi ya kiuchumi inakuja kutoka kwa wadhamini wengine.

Hata hivyo, imeripotiwa na mitandao ya michezo ya Kenya kwamba suala la mgawo wa fedha za klabu bado halijakaa sawa kutokana na kutokamilika kwa mipango ya bajeti ya udhamini.

"Sitaki niseme sana kuhusu ugawo wa klabu, tutajadili kama shirikisho pamoja na wadau na kuangalia bajeti tuliyonayo kabla ya kuliweka wazi suala hilo kwa umma," amesema.

Alipoulizwa kuhusu ruhusa kwa TV za Kenya kujiunga na Azam TV kuonyesha matangazo ya ligi hiyo, Nyamweya alisema suala hilo pia bado linajadiliwa.

Chanzo: MpenjaBlog

kuna watu walisema azam bado sana kwa sababu et dstv amechukua coverage ya kenyan league sasa naona taratibu tunaenda kule tunapohtaji.... imebak ya nigeria ghana congo na south africa wenywe naamin tutafika tu
 
ni hatua nzuri kwa azam nawapongeza kwa jitihada zao, ila wasilete uswahili wa bongo
 
Hongera Azam TV, mwendo mdogo MDOGO! Hadi EPL. Bila shaka strategy zenu ni kuhakikisha mmeuza Ving'amuzi vingi kwenye huu ukanda wa Africa mashariki kabla hamja jitosa kununua Haki ya kuonyesha ligi kuu za Ulaya!!! Big up!!

Klabu zitalamba Kenyan shilling 1 m kila mwezi?? Inamaana ligi yao iko juu kuliko yetu???
Kama sikosei sisi timu zetu zinalamba milioni mia kwa msimu mzima!!
 
Huyu jamaa amedhamiria kweli sema hizi ligi hazina msisimko sana afanye mpango wa EPL,La liga etc.

Big up Azamtv.
 
a very good step that needs apreciation. bado nasubiri ligi kubwa za ulaya hapo ndo ntawakubali kwa 100%. naona dalili za mafanikio hasa baada ya kurekebisha bei za package zao. huwez kupata vitu vizur kwa kulipa 12,500 kwa mwez unless tajir awe anatoa pesa sehem nyingine. natumain hadi kuona epl full tutakuwa tunalipa japo elfu 50-80 kwa mwezi
 
wakenya kwa chuki na wivu wao wa kike dhidi ya watz,usishangae wakija hapa kudai hawatumii ving'amuzi vya azam na wala hiyo azam tv hawaifahamu. Hongera sana azam
 
Ngoja pia tuwawekee watani zetu kwa Kiingereza kama Kiswahili wanajifanya ''hamnazo'' a.k.a hawaelewi kitu

Tanzania-based pay television upstarts Azam Media Limited on Friday announced a three-year broadcast rights partnership worth Sh202 million with Football Kenya Federation Premier League.

The deal will see the 16 clubs in the newly formed FKF PL each receive grants worth Sh10 million annually.

Azam TV CEO Rhys Torrington promised to air at least two matches live on a weekly basis on their sports channels.

“We are keen to turn the sport into a great theatre by broadcasting as much football as we possibly can to Kenyans,” Torrington said during the official announcement in Nairobi yesterday.

“The exposure that comes with airing of matches on TV will play on the back of the players mind and motivate them to perform better. I hope the administrators will use these resources effectively,”Kenya coach Bobby Williamson said.

Seven FKF PL matches are on the card this weekend.

FIXTURES

FKF PL weekend fixtures ( kick offs 3pm)

Saturday – Oserian vs Nakumatt (Naivasha), Agrochemicals vs Zoo Kericho (Moi), Kakamega Homeboys vs St Joseph (Bukhungu), Talanta vs Modern Coast (Nyayo Stadium).

Sunday – Posta Rangers vs Finlays (City), West Kenya vs Nairobi Stima (Bukhungu), Kariobangi Sharks vs Ligi Ndogo (City).

Source: FKF PL, Azam TV sign Sh202m broadcast rights deal - Football - nation.co.ke
 
hatua nzuri kuelekea kutanua soko hapa Afrika Mashariki kabla ya kutuletea uhondo wa ulaya.
 
Long live Azam Media. Najua muda si muda kitu cha EPL kitakuwa mezani
 
Hongera Azam TV, mwendo mdogo MDOGO! Hadi EPL. Bila shaka strategy zenu ni kuhakikisha mmeuza Ving'amuzi vingi kwenye huu ukanda wa Africa mashariki kabla hamja jitosa kununua Haki ya kuonyesha ligi kuu za Ulaya!!! Big up!!

Klabu zitalamba Kenyan shilling 1 m kila mwezi?? Inamaana ligi yao iko juu kuliko yetu???
Kama sikosei sisi timu zetu zinalamba milioni mia kwa msimu mzima!!
aliweka mezani milioni Mia moja kwa kila club mkuu
 
Nchini Uganda Dstv walikwenda mahakamani kupinga lakini mahaka imeibwaga dstv na kuipa haki Azam
 
yote sawa, tisa kumi kwanini timu zetu azipe milioni mia tu kwa mwaka ambayo ni sawa na milioni tano za kenya, halafu wakenya awape milioni mia mbili kwa mwaka sawa na milioni kumi za kenya... Sababu hasa ni nini????????????
 
wakenya kwa chuki na wivu wao wa kike dhidi ya watz,usishangae wakija hapa kudai hawatumii ving'amuzi vya azam na wala hiyo azam tv hawaifahamu.ngoja MK254 aje.hongera sana azam

kadoda11 Mbona uspongeze kama Watanzania wenzio, wewe umejaa uoga kila jina la Kenya linapotajwa. Waje tu wafanye yao, hao ni wafanyi biashara hivyo ina maana patakua na manufaa kwa taifa kiaina.
 
Last edited by a moderator:
Hongera Azam TV, mwendo mdogo MDOGO! Hadi EPL. Bila shaka strategy zenu ni kuhakikisha mmeuza Ving'amuzi vingi kwenye huu ukanda wa Africa mashariki kabla hamja jitosa kununua Haki ya kuonyesha ligi kuu za Ulaya!!! Big up!!

Klabu zitalamba Kenyan shilling 1 m kila mwezi?? Inamaana ligi yao iko juu kuliko yetu???
Kama sikosei sisi timu zetu zinalamba milioni mia kwa msimu mzima!!

Na kumbuka 1Ksh=19Tsh. Hivyo hiyo million moja ya Kenya ni 19m/- za Kitanzania tena kwa mwezi tu!
 
Nchini Uganda Dstv walikwenda mahakamani kupinga lakini mahaka imeibwaga dstv na kuipa haki Azam

Safi sana. Monopoly ya DSTV itapungua kidogo,lakini yule CEO Mzungu na assistant wake Tido D Mhando wanatakiwa wakaze, wakilemaa watapigwa fitina kali sana!
 
yote sawa, tisa kumi kwanini timu zetu azipe milioni mia tu kwa mwaka ambayo ni sawa na milioni tano za kenya, halafu wakenya awape milioni mia mbili kwa mwaka sawa na milioni kumi za kenya... Sababu hasa ni nini????????????

Moja ya sababu ni competition, kama dstv alitoa let say 100m sasa ili ushinde lazima u-bid zaidi ya 100m haijalishi eti kuna ligi Fulani ulidhamini kwa chini au sawa na hiyo amount.
 
Back
Top Bottom