Azam Media yapata haki za kuonesha Ligi Kuu ya Hispania

Rio Tinto

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2014
Posts
777
Reaction score
451

Kupitia ukarasa wao wa Facebook AZAM TV kuanzia tarehe 15 August wataanza kuonyesha mechi za ligi kuu ya Hispania Primera La Liga

Ahsante Azam Tv naamini huu ni mwanzo wa mambo mazuri mengi mno.


 

Attachments

  • azam.png
    36.5 KB · Views: 3,049
Yupo live sasahivi amekuja na kitu kipya, kuanzia mwezi wa 8 ligi ya Spain itaoneshwa live na AZAMTV, pia channel ya Arsenal itaingizwa kwenye decoder soon. Hawa jamaa kweli wamejipanga.
 
CEO wa AZAM TV.Tido Muhando anahojiwa muda huu yupo live akihojiwa na Patrick Nyembera.
Kwamba kuanzia Tarehe 10th August wataonyesha La Liga Liveeeee(Spanish League)

AZAM imepata haki miliki ya kuonyesha Mechi zoote za LA LIGA. TIDO, anasema kwamba alikutana na Uongozi wa La Liga DUBAI,na kuwaambia uwezo wa AZAM TV.
Na haikuwa kazi rahisi kupata Haki miliki kwa kuwa jopo la La Liga lazima lijue uwezo wa Kituo husika na ubora wake.

Ilichukua muda mrefu saana tangu wawasilishe maombI yao, hatimae yamekuwa.

Amegusia tena kuhusu Arsenal TV, wapo kwenye mazungumzo hatua za mwisho na amesema kuna uwezekano wa kupata haki miliki ya kuonyesha mechi zao muda sio mrefu.

Manchester United na Liverpool wapo kwenye mazungumzo na yanaendelea vizuri.

Amegusia Tena Kuhusu EPL, wapo kwenye mazungumzo nao, Uongozi mkuu wa AZAM TV ulitoka na kuwafuata viongozi wa EPL UK.

TIDO anakiri kwamba ni kazi kubwa zaidi kwa hili,lakini amesema watafika hatua nzuri tu.

AZAM TV ndio habari ya MJINI
 
Wooooow!!!hii ni habari njema sana kwangu mimi mpenzi wa la liga,dstv bye bye,nilikuwa bado natafakari hii 200,000 yao nitakuwa nailipaje.well done Azamtv.sasa nimeamini mmeamua na mmedhamiria kweli kumtimua beberu.
 
Waambie WasituDstv kwenye bei. !
Hahahah,mkuu bei zitakuwa za kawaida sana licha ya kwamba badi zipo chini ya Carpet.
Maana target yao ni kutangaza biashara zao,ila hao wengine kwao ni sehem ya mapato.
Kwahiyo acha tutegemee bei nzuri mkuu.

Maana hata Pre Season Matches za Liverpool zinaonyeshwa Live siku hizi kupitia AZAM TV Channel ya Liverpool Tv.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…