Azam Media yapata haki za kuonesha Ligi Kuu ya Hispania

Azam Media yapata haki za kuonesha Ligi Kuu ya Hispania

Itakuwa ni mara ya kwanza kwa vituo vya sehemu hii ya Afrika kuwa na matangazo haya na iwapo ndivyo Tido Dunsturn Muhando na kampuni ya Azam wana haki ya kuwa juu , sijui kama itakuwaje naogopa isijekuwa tena huko mbele tunauziwa vifurushi kwa bei za Dola Chonde chole wandugu
 
Ni vizuri kujua kama mech moja kwa au mech zote? Maana isije ilawa wamempangia mechi,na LA LIGA wapo chini ya sky sport
 
Kwenye bei sasa....btw tunafurahi mswahili kuthubutu na anaelekea kuwatoa jasho makabaila.....
 
Ni vizuri kujua kama mech moja kwa au mech zote? Maana isije ilawa wamempangia mechi,na LA LIGA wapo chini ya sky sport

Wamesema mechi zote....hata dogo Edo Kumwembe katangaza mechi zote kuoneshwa....
 
Mimi niupongeze sana uongozi wa Azam media kwa habari njema ihi,nimafanikio makubwa sana kwa kampuni ihi.

Watanzania wengi wenye uwezo mdogo wa kipato imekua ni ngumu wao kupata burudani haswa mipira,

kume kuwepo na makampuni mengi ya vingamuzi na yenye uwezo mkubwa kama (startimes) lakini habari za mipira kwo imekua ni hadithi na kuunga unga,

hakika vingamuzi vya azam tv sasa zitaanza kununuliwa kama njugu,maana ihi ni habari njema sana kwa wapenda soka

ila angalizo hatakama watapandisha gharama basi waangalie na hali za wananchi wasi waumize sana,
 
Ya itakuwa kheri sana dstv walikuwa hawana mpinzani hayo ndio mambo mazuri tunayoyataka
 
Kwa habari hii, sasa nitanunua kisimbusi cha AZAM. Jamani nauza kisimbusi cha DStv kwa anaehitaji. Nimewatajirisha hawa wajng vya kutosha.
Tido oyee,
Mzee Said Mohamed Oyee,
Mkulu Bakhresa Oyee
 
Hongera sana!tatizo hapa tz hata tvs nyingi zina elements za ki- siasa,..azam mnaonyesha mwanga mpya...hata wale wa radio E fm nao wakaze buti sana ili kuleta mapinduzi nawapenda sana ktk uchambuzi wa soka
 
Dstv lazime wachanganyikiwe

Yaani nimeshawachukia sana DStv...wapuuzi sana, kila siku kupandisha bei.

Ngoja nifanye utaratibu wa kununua AZAM TV decoder...La Liga si yakuikosa kabisa.
 
Mimi sio mpenzi wa La Liga ila ni kada wa EPL tangu enzi za David Ginola, Paul Wanchope, Andy Cole nk. So, Wakipata hati miliki ya EPL nitanunua king'amuzi chao. DSTV bei yao iko juu sana, sawa na kodi ya nyumba bwana!!!
 
Back
Top Bottom