PROSPER 05
JF-Expert Member
- Oct 14, 2013
- 226
- 217
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Azam ni kwamba Hernandez amewaambia mabosi wa timu hiyo kuwa anataka kuwa na kikosi ambacho kitatisha
KOCHA Mhispanyola wa Azam, Zeben Hernandez amechoshwa na dhihaka ya kufungwa na timu za kawaida kama Mbao FC na Ndanda na sasa alichokifanya klabuni hapo ni tetemeko pengine kama lile lililotokea pale Kagera.
Azam imeanza kukisuka upya kikosi chake chini ya Hernandez ambapo tayari imesajili mastraika wawili kutoka Ghana ambao ni Samuel Afful na Yahya Mohammed pamoja na winga Enock Agyei na sasa inapambana kuongeza nguvu katika maeneo mengine.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Azam ni kwamba Hernandez amewaambia mabosi wa timu hiyo kuwa anataka kuwa na kikosi ambacho kitatisha katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani na pia kurejesha heshima Ligi Kuu Bara.
Mabingwa hao kwa sasa wanasaka wachezaji wanne wazawa ambao ni beki mmoja, kiungo mmoja na mshambuliaji mmoja. Katika tafuta hao winga Hassan Kabunda wa Mwadui pamoja na mshambuliaji Ludovic Venance wa Mbao FC tayari wameingia katika rada zao na wanaweza kusaini muda wowote.
Wachezaji ambao wanapunguzwa ili kupisha damu mpya ni Waivory Coast, Kipre Bolou na Gonazo Bi Ya Thomas ambao wanaungana na Sergie Wawa aliyetimkia El Merreikh ya Sudan kupisha ujio wa nyota watatu kutoka Ghana.
Kwa upande wa wachezaji wazawa, panga limepita kwa mshambuliaji Hamis Mcha pamoja na beki Ismail Gambo ambaye alirejeshwa klabuni hapo mapema msimu huu.
Hata hivyo bado mjadala mkubwa unaendelea kuona kama atapatikana beki makini kutoka nje ambaye ataziba nafasi ya Wawa ambapo kama itakuwa hivyo basi kiungo, Jean Mugiraneza ‘Migi’ atapewa mkono wa kwaheri.
Mwanaspoti:
Go! go! Azam Gooo!. Hakuna kusajili kwa mazoea wala Historia...