Azam mpya itawalaza na viatu

Azam mpya itawalaza na viatu

PROSPER 05

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2013
Posts
226
Reaction score
217
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Azam ni kwamba Hernandez amewaambia mabosi wa timu hiyo kuwa anataka kuwa na kikosi ambacho kitatisha

KOCHA Mhispanyola wa Azam, Zeben Hernandez amechoshwa na dhihaka ya kufungwa na timu za kawaida kama Mbao FC na Ndanda na sasa alichokifanya klabuni hapo ni tetemeko pengine kama lile lililotokea pale Kagera.

Azam imeanza kukisuka upya kikosi chake chini ya Hernandez ambapo tayari imesajili mastraika wawili kutoka Ghana ambao ni Samuel Afful na Yahya Mohammed pamoja na winga Enock Agyei na sasa inapambana kuongeza nguvu katika maeneo mengine.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Azam ni kwamba Hernandez amewaambia mabosi wa timu hiyo kuwa anataka kuwa na kikosi ambacho kitatisha katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani na pia kurejesha heshima Ligi Kuu Bara.

Mabingwa hao kwa sasa wanasaka wachezaji wanne wazawa ambao ni beki mmoja, kiungo mmoja na mshambuliaji mmoja. Katika tafuta hao winga Hassan Kabunda wa Mwadui pamoja na mshambuliaji Ludovic Venance wa Mbao FC tayari wameingia katika rada zao na wanaweza kusaini muda wowote.

Wachezaji ambao wanapunguzwa ili kupisha damu mpya ni Waivory Coast, Kipre Bolou na Gonazo Bi Ya Thomas ambao wanaungana na Sergie Wawa aliyetimkia El Merreikh ya Sudan kupisha ujio wa nyota watatu kutoka Ghana.

Kwa upande wa wachezaji wazawa, panga limepita kwa mshambuliaji Hamis Mcha pamoja na beki Ismail Gambo ambaye alirejeshwa klabuni hapo mapema msimu huu.

Hata hivyo bado mjadala mkubwa unaendelea kuona kama atapatikana beki makini kutoka nje ambaye ataziba nafasi ya Wawa ambapo kama itakuwa hivyo basi kiungo, Jean Mugiraneza ‘Migi’ atapewa mkono wa kwaheri.
Mwanaspoti:

Go! go! Azam Gooo!. Hakuna kusajili kwa mazoea wala Historia...
azam-.jpg
 
Yanga silent killer anawaangalia tu sarakasi zenu mara okwi mara kabunda
Yanga mwendo ni ule uleee
 
Unamaanisha nini unaposema hamsajili kwa historia?twende taratibu,nijibu
 
Nilitarajia makubwa kutoka Azam but nimegundua Mswahili ni mswahili tu!! Haitakaa itoboe maana naona sahiz imebaki bure kama mwadui
 
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Azam ni kwamba Hernandez amewaambia mabosi wa timu hiyo kuwa anataka kuwa na kikosi ambacho kitatisha

KOCHA Mhispanyola wa Azam, Zeben Hernandez amechoshwa na dhihaka ya kufungwa na timu za kawaida kama Mbao FC na Ndanda na sasa alichokifanya klabuni hapo ni tetemeko pengine kama lile lililotokea pale Kagera.

Azam imeanza kukisuka upya kikosi chake chini ya Hernandez ambapo tayari imesajili mastraika wawili kutoka Ghana ambao ni Samuel Afful na Yahya Mohammed pamoja na winga Enock Agyei na sasa inapambana kuongeza nguvu katika maeneo mengine.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Azam ni kwamba Hernandez amewaambia mabosi wa timu hiyo kuwa anataka kuwa na kikosi ambacho kitatisha katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani na pia kurejesha heshima Ligi Kuu Bara.

Mabingwa hao kwa sasa wanasaka wachezaji wanne wazawa ambao ni beki mmoja, kiungo mmoja na mshambuliaji mmoja. Katika tafuta hao winga Hassan Kabunda wa Mwadui pamoja na mshambuliaji Ludovic Venance wa Mbao FC tayari wameingia katika rada zao na wanaweza kusaini muda wowote.

Wachezaji ambao wanapunguzwa ili kupisha damu mpya ni Waivory Coast, Kipre Bolou na Gonazo Bi Ya Thomas ambao wanaungana na Sergie Wawa aliyetimkia El Merreikh ya Sudan kupisha ujio wa nyota watatu kutoka Ghana.

Kwa upande wa wachezaji wazawa, panga limepita kwa mshambuliaji Hamis Mcha pamoja na beki Ismail Gambo ambaye alirejeshwa klabuni hapo mapema msimu huu.

Hata hivyo bado mjadala mkubwa unaendelea kuona kama atapatikana beki makini kutoka nje ambaye ataziba nafasi ya Wawa ambapo kama itakuwa hivyo basi kiungo, Jean Mugiraneza ‘Migi’ atapewa mkono wa kwaheri.
Mwanaspoti:

Go! go! Azam Gooo!. Hakuna kusajili kwa mazoea wala Historia...
View attachment 436432

Kama kuna mistake Ambayo Azam wameifanya basi ni kumuacha Sergie Wawa. Huyo jamaa ni bonge la Mchezaji
 
Wawa namkubali sana Lakini mpaka mkataba unaisha ajaitumikia Azam kwa zaidi ya miezi 6 ni majeruhi na nafasi ya wachezaji wa kigeni ni 7 tu. unafikiri kulikua na sababu ya kumuongezea mkataba?
 
Tatizo la azam sio wachezaji tatizo lao kufukuza walimu ovyoovyo
 
Azam wanakosa watu wa maana ijapo wana kila kitu
 
Tatizo la azam sio wachezaji tatizo lao kufukuza walimu ovyoovyo
Walimu wanaondolewa na Vipengere vya mikataba wanayosaini wao wenyewe. Mfano
  • Umekuta timu inashiriki kimataifa hivyo Hakikisha Mwisho wa Ligi timu inaendelea kupata nafasi ya Kushiriki Kimataifa kwa Mwaka ujao
  • Timu ifike hatua ya Makundi shirikisho,
Then kocha Anaeleza Mahitaji yake, anapatiwa resources zote, anapewa fursa ya Kufanya usajili bila kuingiliwa.
 
Azam wana mawenge, mwaka huu ni wasindikizaji
 
Timu ya kiwanda inaenda kuwa kama mtibwa sukari.... Kosa walivyomfukuza jemedari waliobaki mazazwa hawajui Fitna ya mpira wa bongo
 
Mimi nlidhani azam kaanzisha bendi....kumbe hao ni wachezaji?!
 
Back
Top Bottom