Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,896
- 4,058
Yanga na Simba huwa wanacheza huku wamevaa jezi za SportPesa na wanaonyesha mechi zao zote. Ligi ya Spain na Uingereza kuna timu kibao zinavaa jezi zilizodhaminiwa na makampuni ya betting na bado wanaonyesha hizo ligi bila tashwishwi yoyote.
Jana kwenye mchezo wa ngumi, Mwakinyo ameeleza baada ya mchezo kuwa ilimbidi abadilishe gloves zenye lebo ya SportPesa ikiwa ni sharti alilopewa na warushaji wa mchezo huo Azam TV.
Mwakinyo kaeleza kuwa gloves alizobadilishiwa zilimpa shida kwani hajazizoea. Sote tunajua pia kwamba Azam huwa hawaonyeshi mashindano ya SportPesa yanayoshirikisha timu za Kenya na Tanzania kwa kisingizio hicho hicho cha dini.
Labda ndugu zetu Waislamu watatusaidia, hivi maelezo ya kukataza michezo ya kamali yanabagua kama wanavyofanya hawa jamaa?
Pia Azam kupitia UTV wamekua wakionyesha nyimbo za mziki wa kisasa huku mabinti wakiwa wamevaa vichupi na vinguo vifupi kabsa; je hayo ni maadili ya dini?
Ninachokijua mimi michezo yote kwa sasa inaendeshwa na fedha chafu za makampuni ya pombe, kamali, sigara, kondom n.k. Kama ukitaka kukwepa dhambi zitokanazo na najsi hiyo, basi usifanye kabisa biashara ya michezo hasa kuonyesha mechi. La sivyo nikujichanga kiimani tu.