Azam na SportPesa: Ni kweli imani ndiyo kikwazo?

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Yanga na Simba huwa wanacheza huku wamevaa jezi za SportPesa na wanaonyesha mechi zao zote. Ligi ya Spain na Uingereza kuna timu kibao zinavaa jezi zilizodhaminiwa na makampuni ya betting na bado wanaonyesha hizo ligi bila tashwishwi yoyote.

Jana kwenye mchezo wa ngumi, Mwakinyo ameeleza baada ya mchezo kuwa ilimbidi abadilishe gloves zenye lebo ya SportPesa ikiwa ni sharti alilopewa na warushaji wa mchezo huo Azam TV.

Mwakinyo kaeleza kuwa gloves alizobadilishiwa zilimpa shida kwani hajazizoea. Sote tunajua pia kwamba Azam huwa hawaonyeshi mashindano ya SportPesa yanayoshirikisha timu za Kenya na Tanzania kwa kisingizio hicho hicho cha dini.

Labda ndugu zetu Waislamu watatusaidia, hivi maelezo ya kukataza michezo ya kamali yanabagua kama wanavyofanya hawa jamaa?

Pia Azam kupitia UTV wamekua wakionyesha nyimbo za mziki wa kisasa huku mabinti wakiwa wamevaa vichupi na vinguo vifupi kabsa; je hayo ni maadili ya dini?

Ninachokijua mimi michezo yote kwa sasa inaendeshwa na fedha chafu za makampuni ya pombe, kamali, sigara, kondom n.k. Kama ukitaka kukwepa dhambi zitokanazo na najsi hiyo, basi usifanye kabisa biashara ya michezo hasa kuonyesha mechi. La sivyo nikujichanga kiimani tu.
 
Ndiyo walimnyima ushindi wa knockout Mwakinyo maana zile gloves alizotoka nazo zina miezi kadhaa zilikuwa kwa Babu......jana waliharibu kabisa masharti ya mganga (Utani tu)
 
Hili ni kosa kwani kama ni dini hata kupigana kichwani hairuhusiwi
Kama ni dini wanajichanganya kwa kweli
 
Siku hizi naona anaajiri na kina Peter,John na wabantu pia.
 
Kumbuka hata jamiiforum ni biashara ya mtu! Unaweza kujifanya mjuaji kumbe ndo lyapukile kabsa
Mimi nadhani unge fuata biashara yako na si kuchunguza za mwanaume mwenzio.
Azam ni mali yake kwa hiyo anaweza kuiendesha anavyo taka.
 
Kwakuwa Azam hawajasema hayo ila ni wewe mwenyewe umefikiria hivyo basi komaa na mawazo yako ukipata jibu mpelekee TIDO.
Swala halikuwa dini ila nembo ya biashara nyingine wakati wao ndio wamebeba lile pambano lote kama wadhamini.
 
Yanga na Simba huwa wanacheza huku wamevaa jezi za SportPesa na wanaonyesha mechi zao zote. Ligi ya Spain na Uingereza kuna timu kibao zinavaa jezi zilizodhaminiwa na makampuni ya betting na bado wanaonyesha hizo ligi bila tashwishwi yoyote.

Jana kwenye mchezo wa ngumi, Mwakinyo ameeleza baada ya mchezo kuwa ilimbidi abadilishe gloves zenye lebo ya SportPesa ikiwa ni sharti alilopewa na warushaji wa mchezo huo Azam TV.

Mwakinyo kaeleza kuwa gloves alizobadilishiwa zilimpa shida kwani hajazizoea. Sote tunajua pia kwamba Azam huwa hawaonyeshi mashindano ya SportPesa yanayoshirikisha timu za Kenya na Tanzania kwa kisingizio hicho hicho cha dini.

Labda ndugu zetu Waislamu watatusaidia, hivi maelezo ya kukataza michezo ya kamali yanabagua kama wanavyofanya hawa jamaa?

Pia Azam kupitia UTV wamekua wakionyesha nyimbo za mziki wa kisasa huku mabinti wakiwa wamevaa vichupi na vinguo vifupi kabsa; je hayo ni maadili ya dini?

Ninachokijua mimi michezo yote kwa sasa inaendeshwa na fedha chafu za makampuni ya pombe, kamali, sigara, kondom n.k. Kama ukitaka kukwepa dhambi zitokanazo na najsi hiyo, basi usifanye kabisa biashara ya michezo hasa kuonyesha mechi. La sivyo nikujichanga kiimani tu.

Ni unafiki tu wa kuchagua dhambi...raia anaponda kitimoto wakati anakula mombe na washeli.
 
Wana sema hawakubaliani na kampuni za betting mkuu
Walisema Wapi? Acheni kupotosha.
La Liga Santander ina timu kibao zinadhaminiwa na Makampuni ya betting, mbona wanaonyesha? Issue ni hiyo tu kua ukionyesha biashara ya mtu akulipe basi.

Lakini hili swala lilifaa lijadiliwe na kukubaliana kabla ya hata ya kusainisha contract. Mwakyinyo anasema Sportpesa ni wadhamini wake, Sasa utakataaje wadhamini dakika ya mwisho? Isitoshe pia biashara ya Azam haifanani na biashara ya Sportpesa, huwezi kukataa.

Au Mwakyinyo hakuwaambia Azam kua yeye anadhaminiwa na Sportpesa?
 
Back
Top Bottom