Uchumi wa kati wa Tanzania umeshindwa kuwa na makampuni makubwa kudhamini mechi hii kupitia Azam TV.
Channel nyingi kimataifa hutafuta hutafuta mdhamini atakayegharamia kulipia leseni ya muda kurusha matangazo kwa wenye haki na pia kugharamia gharama za Azam TV kuwezesha kurusha mechi.
Kampuni za bia, Mobile Phone, mabenki n.k ya Tanzania vipi uchumi wenu mdogo hata kugharamia matangazo ? Azam TV haiwezi kubeba gharama hizo bila kuwepo mdhamini kwa mkataba maalum.
Chaneli za michezo kama za Super sports, channel za uarabuni, South Africa, Ulaya Marekani ya Kaskazini ESPN n.k hushirikiana na makampuni kudhamini na kuufanikisha kurushwa matangazo ya michezo na siyo vinginevyo kuwa vituo vya Televisheni kubeba mzigo wote.
Na ndiyo maana tunaona Michezo inaendelea kurusha live ktk TV bila watazamaji uwanjani kipindi hiki cha Covid -19 kwani nyuma ya "pazia" vituo hivyo vya TV kuna wadhamini wakubwa yaani makampuni wanagharamia zoezi hilo ili makampuni hayo yajitanue kibiashara, kuongeza mauzo ya bidhaa / huduma za wadhamini kufahamika n.k.