[QUOTE="sembo]
Huku akishuhudiwa na mashabiki lukuki waliofurika katika uwanja wa Jamuhuri, uliopo mjini Morogoro.. Yule Mnyama hatari mwituni, Simba S.C aunguruma tena.
Na hii ni baada ya kuwakung'uta bila huruma, goli 3-0 Bukina Faso.
Mechi hii ilikua ni ya kuwania Kombe la Shirikisho.. Walioacha kilio kikubwa kilichojaa simanzi nyingi kwa mashabiki wa Bukina Faso na Ndala, katika mji kasoro bahari, Moro ni Hamis Kiiza [dk.78 na dk. 90] na Mwinyi Kazimoto a.k.a Ball Dancer [dk. 90].
Japo mashabiki wa Bukina Faso na Ndala wametoka wakiwa vichwa chini.. Ila wameshindwa kabisa kuficha chuki zao kwa Mnyama na kuanza kulisifia soka maridadi walilotandaza leo vijana wa Mayanja.. Kwa kifupi hapa mjini Moro... Leo ni Simba S.C kila kona.
Jackson Mayanja.
Katika mechi zake 3 alizoiongoza Simba S.C kama Kocha Mkuu.. Timu imeshinda mechi 3.. Imefunga magoli 6.. Imefugwa magoli 0.
Naziona neema zinakuja.. Chini ya Mayanja
[/QUOTE]
Goooo