Azam TV boresheni kamera zenu

Azam TV boresheni kamera zenu

Singasinga

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2011
Posts
2,711
Reaction score
3,279
Habari wakuu,

Kwa tukio la jana kukataliwa goal la Geita Gold ni wazi Azam TV wanapaswa kuboresha eneo lao la camera kwani hawakupi nafasi ya kuangalia angle zote za move ya mpira.

Mfano jana kwa picha za marudio zinaonesha tu kapombe akianguka na mfungaji kupiga kichwa na goal kukataliwa.

Je Kapombe aliwaza tu kuanguka mbele makusudi kama amepata ugonjwa wa kifafa au tatizo la moyo? kuna kitu kilitokea ambacho uduni wa camera za Azam ulitunyima kukiona.

Na ninafikiri mwamuzi alipaswa kutoa na card kwa mfungaji kwa kuhatarisha maisha ya kapombe maana rafu ya kutokea nyuma huwa ni mbaya sana.
 
simba wanaifanya ligi hii ya nbc ionekane ndiyo 'most corrupted league' kwenye sayari hii, alafu ile taasisi ya kupambana na rushwa sijui inafanyaga kazi ganii??
 
Hawakugusana hata kidogo kapombe alianguka mwenyewe baada ya kuukosa mpira hapo tutasingizia camera
 
Kwa tukio la jana baada ya kuangalia replay ni ngumu kusema kuwa Kapombe aliangushwa na mchezaji wa Geita kutokaba na umbali walioachana hao wachezaji. Wameachana umbali mkubwa sana hivyo hakuna mgusano wowote.
 
Kwani Fei toto kwa namungo alifanyeje? Vitu vinavouwa mpira wa bongo ni vitatu (1)TFF (2)SIMBA (3)YANGA ukiwadhibiti hao kutakuwa soka bora na ni kitu hakiwezekani.
 
Nishaachana na league ya kifala Kama hii ....

League gani inatimu mbili tu ..yaani Simba na yanga hazitaki kufugwa
 
Kapombe alisukumwa hapa na mfungaji kabla ya mpira kumfikia mfungaji.
Ni faulo ya wazi kabisa
Screenshot_20211202-091234_Lite.jpg
 
Kuna matukio mengi yanatokea wakati wa mchezo ambayo camera za Azam tv inashindwa kuyaweka clear hivyo kubaki na utata mwingi kujua kipi ni kipi.

Azam tv ni muda sasa muongeze ubora katika hilo eneo ili matukio yawe clear hata kama mwamuzi anapuyanga tujue kapuyanga 100%.

Mfano ile penati ya Simba vs Mbao Fc fainali ya kombe la F.A. Hadi leo ukiifatilia ile video utagundua Azam tv bado kunachangamoto kubwa sana "kwenye matukio ya utata" camera zao hazitusaidii.
 
Binafsi nilivyoona ni kwamba camera haikuonyesha tukio zima, camera zimeanza kunasa baada ya kuruka na si kabla.
Ni wazi kwamba Kapombe alisukumwa, hakuna namna mtu anaweza kuruka juu kutoka point A na kwenda kuangukia point B.

For me, it’s a clear foul.
 
Habari wakuu,

Kwa tukio la jana kukataliwa goal la Geita Gold ni wazi Azam TV wanapaswa kuboresha eneo lao la camera kwani hawakupi nafasi ya kuangalia angle zote za move ya mpira.

Mfano jana kwa picha za marudio zinaonesha tu kapombe akianguka na mfungaji kupiga kichwa na goal kukataliwa.

Je Kapombe aliwaza tu kuanguka mbele makusudi kama amepata ugonjwa wa kifafa au tatizo la moyo? kuna kitu kilitokea ambacho uduni wa camera za Azam ulitunyima kukiona.

Na ninafikiri mwamuzi alipaswa kutoa na card kwa mfungaji kwa kuhatarisha maisha ya kapombe maana rafu ya kutokea nyuma huwa ni mbaya sana.
Kwanza kabisa ww ni msimbazi
 
Matukio ya kimcharuko kama haya yanaathiri matokeo ya timu. Hivyo kuongeza Camera tu hakutoshi maana maamuzi ya Refa hayabadilishwi. Tuliyaona pia kwenye mechi ya Yanga vs Ruvu, Yanga vs Azam, Yanga vs Namungo, Pia Yanga vs Mbeya Kwanza.

Tiba nzuri ni kuwa na matumizi ya VAR au Azam waweke Tv uwanjani maalum kwa Refa kwenda kuangalia Replay iwapo kutatokea utata wowote kisha afanye maamuzi hapo hapo uwanjani.
 
Kapombe alisukumwa hapa na mfungaji kabla ya mpira kumfikia mfungaji.
Ni faulo ya wazi kabisa
View attachment 2030162
Hakuna camera yoyote ya Azam inayoonesha tukio la video kwa namna hiyo. Hizo ni picha mgando zinazosambazwa na mashabiki mitandaoni. Baada ya kuona kuona hii picha yako ilinifanya niingie youtube pengine nitakutana na mgusano wa namna hiyo ili nijiridhishe kuwa kuna mgusano ila cha ajabu nakuta mtu kaweka caption ya video ya namna hiyo halafu ukija ku play ili uone. Unakuta video haioneshi kama alivyoiweka caption ya picha mnato. Kama uamini basi tafuta hiyo video halafu inaonesha tukio kama ilivyo kwenye hiyo picha ilivyoonesha iweke hapa hiyo video. Utatafuta hauwezi kuipata video ya hiyo picha iliyopostiwa hapo.

Kuna mapungufu kwa upande wa camera za Azam hilo lipo wazi kuna utata mwingine wa offside inatakiwa uamuliwe kwa camera za angle tofauti tofauti lakini pia wanaokataa mchezaji hawezi kudondoka mwenyewe basi sio wafuatiliaji wa mipira. Mchezaji anaweza kuruka juu kisha akarudi chini vibaya. Sijasema kama Kapombe hakuchezewa faulo au lah. Ila nachoona kwenye replay zote ni kwamba hakuna physical contact baina yao na wameachana kwa umbali
 
Back
Top Bottom