XII Tz
JF-Expert Member
- Aug 16, 2020
- 4,345
- 7,076
Inawezekanaje mtu akaruka juu alafu akabadili muelekeo akiwa angani na kuangukia mita kadhaa mbele bila kusukumwa? .. inaingia akilini kweli ?Hakuna camera yoyote ya Azam inayoonesha tukio la video kwa namna hiyo. Hizo ni picha mgando zinazosambazwa na mashabiki mitandaoni. Baada ya kuona kuona hii picha yako ilinifanya niingie youtube pengine nitakutana na mgusano wa namna hiyo ili nijiridhishe kuwa kuna mgusano ila cha ajabu nakuta mtu kaweka caption ya video ya namna hiyo halafu ukija ku play ili uone. Unakuta video haioneshi kama alivyoiweka caption ya picha mnato. Kama uamini basi tafuta hiyo video halafu inaonesha tukio kama ilivyo kwenye hiyo picha ilivyoonesha iweke hapa hiyo video. Utatafuta hauwezi kuipata video ya hiyo picha iliyopostiwa hapo.
Kuna mapungufu kwa upande wa camera za Azam hilo lipo wazi kuna utata mwingine wa offside inatakiwa uamuliwe kwa camera za angle tofauti tofauti lakini pia wanaokataa mchezaji hawezi kudondoka mwenyewe basi sio wafuatiliaji wa mipira. Mchezaji anaweza kuruka juu kisha akarudi chini vibaya. Sijasema kama Kapombe hakuchezewa faulo au lah. Ila nachoona kwenye replay zote ni kwamba hakuna physical contact baina yao na wameachana kwa umbali