Hawa jamaa wanaboa sana. Kwa mfano katika mechi ya Yanga na Mafunzo, pale Yanga walipofanya makosa walikuwa wanawabeza Mafunzo kwamba hawako vizuri na kudai eti kama Yanga angecheza na timu bora kama Azam asingesalimika kwa kosa lile.
Mechi yao (Azam) ilipoanza kuchezwa wakacheza mchezo mbovu kuliko hata wa Mafunzo. Shame on you Azam TV, hatuna jinsi tu vinginevyo tungekuwa tumeshawatosa siku nyingi sana.
Nimegundua kaujanja haka: Ili kuepuka porojo za hawa jamaa, ondoa sauti ya TV kisha angalia picha tu huku ukisikiliza muziki wa injili kwa sauti ya chini katika redio, inaleta raha zaidi kuliko kusikiliza utumbo wa hawa jamaa. Kama siyo mpenzi wa muziki wa injili weka muziki unaoupenda ili mradi usisikie utumbo wao!