Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Bondia Twaha Kiduku amethibitisha kuwa Azam Media haitarusha michezo ya masumbwi tena kutokana na mashtaka yaliyofunguliwa. Amepongeza Azam Media kwa mchango wake mkubwa katika kukuza michezo na sanaa nchini, akitaja kwamba kupitia Azam TV, michezo na vipaji vya vijana vimeimarika na kuleta ajira. Hata hivyo, amewashauri wanamichezo kukaa pamoja ili kutatua changamoto na kuepuka madhara kwa tasnia.
Azam media imekuwa chachu ya kunyanyua Sanaa na michezo nchini, Kupitia Azam tv leo hii tuna ligi bora ya mpira wa miguu, tamthilia zimerudi kwa kasi, lakini pia kwa upande wa mchezo wetu wa masumbwi umekuwa mkubwa, kupitia Azam tv vijana wengi tumepata ajira na tumeajiri vijana wenzetu na watu wengine wengi kwasababu ya matunda tuliyovuna kupitia vipaji vyetu ambavyo vimeonekana kupitia Azam tv, hivyo ombi langu kwa wanamichezo Kama Kuna dosari inatokea ya aina yoyote inatokea baina ya Azam tv nasisi Kama wa wanamichezo tujaribu kukaa chini kwa pamoja na kutatua changamoto hizo kwani tukiruka hatua kubwa tunaweza kusababisha madhara kwa vizazi na vizazi na kupoteza tasnia nzima ya mchezo wetu pendwa, tujifunze kupitia wenzetu wa mpira wa miguu na maigizo, sio kwamba hawapati changamoto Ila wanatatua ili kuweka sawa kesho yao.
Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Patrick Kahemele, amefafanua sababu za Azam kutoonyesha mchezo wa Masumbwi.
Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Patrick Kahemele, amefafanua sababu za Azam kutoonyesha mchezo wa Masumbwi.