Bondia Twaha Kiduku amethibitisha kuwa Azam Media haitarusha michezo ya masumbwi tena kutokana na mashtaka yaliyofunguliwa. Amepongeza Azam Media kwa mchango wake mkubwa katika kukuza michezo na sanaa nchini, akitaja kwamba kupitia Azam TV, michezo na vipaji vya vijana vimeimarika na kuleta ajira. Hata hivyo, amewashauri wanamichezo kukaa pamoja ili kutatua changamoto na kuepuka madhara kwa tasnia.
Your browser is not able to display this video.
Azam media imekuwa chachu ya kunyanyua Sanaa na michezo nchini, Kupitia Azam tv leo hii tuna ligi bora ya mpira wa miguu, tamthilia zimerudi kwa kasi, lakini pia kwa upande wa mchezo wetu wa masumbwi umekuwa mkubwa, kupitia Azam tv vijana wengi tumepata ajira na tumeajiri vijana wenzetu na watu wengine wengi kwasababu ya matunda tuliyovuna kupitia vipaji vyetu ambavyo vimeonekana kupitia Azam tv, hivyo ombi langu kwa wanamichezo Kama Kuna dosari inatokea ya aina yoyote inatokea baina ya Azam tv nasisi Kama wa wanamichezo tujaribu kukaa chini kwa pamoja na kutatua changamoto hizo kwani tukiruka hatua kubwa tunaweza kusababisha madhara kwa vizazi na vizazi na kupoteza tasnia nzima ya mchezo wetu pendwa, tujifunze kupitia wenzetu wa mpira wa miguu na maigizo, sio kwamba hawapati changamoto Ila wanatatua ili kuweka sawa kesho yao.
Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Patrick Kahemele, amefafanua sababu za Azam kutoonyesha mchezo wa Masumbwi.
Huyo mwamakula hana haki ya mchezo mzima wa masumbwi, kama ni haki ya jina azam wanaweza kutumia jina lingine na mchezo wa masumbwi ukaendelea kuoneshwa. Labda iwe ni suala la udini wa mmiliki.
Huyo mpuuzi anakwenda kurudisha watu nyuma kimaisha hasa mabondia, n wapumbavu pekee ndio hawatoona mchango wa Azam Media kwenye masuala ya michezo hapa nchini.
Azam Media wamepeleka michezo mingi ya Tz mbele mno, leo hii wachezaji wa magharibi wote wanatamani kuja kucheza Tz hii yote n kutokana na mchango wa Azam Media.