CORE i15
New Member
- Sep 14, 2018
- 3
- 1
Niende moja mwa moja kwenye pointi.
Kampuni ya Azam Media ni kati ya kampuni ambazo zinahitaji marekebisho makubwa sana kwenye idara ya huduma kwa wateja. Kwanza kabisa mteja kwao si mfalme kabisa yaani wanatreat wateja kama vile wanatoa huduma yao bure.
Ni siku ya pili sasa ukijaribu kulipia kifurushi chochote kinagoma, wameweka namba zao za hudumu kwa wateja ila zinaita tu na kuna muda ziko busy iwe usiku au mchana. Mbaya zaidi watu wanalalamika katika page zao za social media lakini hakuna majibu.
Kiustaarabu wangetoa majibu yanayoeleweka kwa walaji au wateja wao ili tujue kuna shida gani ila kukaa kimya ni moja kati ya dharau kubwa sana kwa wateja wake.
Kama kuna muhusika humu naomba tafadhali sana toeni majibu kwa wateja wenu kama kuna shida tujue. Jifunzeni kwa wenzenu DStv.