Mimi ving'amuzi vya kiswahili haviwezi hata kwa bunduki kukanyaga nyumbani kwangu.
Kuna siku nimeenda mahala shemeji yangu ana ki-grocery ameweka azam, ikafika kipindi cha mpira akaniomba niwapigie azam, nikapiga hawapokei, nikarudia mara kadhaa wakapokea ila wakanipa majibu ya hovyo hovyo kanla sijamaliza hata kuuliza wakakata simu.
Mimi hata bure azam na startimes situmii ingawa startimes kipo(hiki nilinunua sababu bimkubwa alikua anapenda itv) ikanilazimu nikinunue, baada ya hapo nimekitupia stoo.
Dstv bana, hata sa 3 usiku unapiga simu wanakuhudumia, hata ukiwadanganya umelipia ila hawajaona malipo yako wanakurejeshea huduma ingawa baada ya masaa kadhaa itaondoka kama hujalipa kweli, wanavitengo vya huduma kwa wateja, vip, normal customers.
Watanzania wenzangu lazima tukubali kua vya bure ni gharama na hasara.