Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #21
#MorningTrumpet ni laivu kila siku asubuhi hairudiwagi.
WildCard,
Marudio wamenifahamisha ni leo saa tano usiku.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
#MorningTrumpet ni laivu kila siku asubuhi hairudiwagi.
#MorningTrumpet ni laivu kila siku asubuhi hairudiwagi.
Iwe mbali kabisa na historia ya TANU au ya NCHI. TANU haikuwa ya WaIslam wala NCHI hii sio ya WaIslam au DINI nyingine yoyote.

Mbona unamdanganya mwenzako kuwa kipindi hakirudiwi.#MorningTrumpet ni laivu kila siku asubuhi hairudiwagi.
Kikirudiwa kinaitwaje tena?Mbona unamdanganya mwenzako kuwa kipindi hakirudiwi.
Cha Waislam kilikuwa AMNUTWildCard,
Kuhusu TANU kuwa chama kilichokuwa kwa Waislam suala hili tumejadili sana
hapa Majlis halikadhalika jinsi Kanisa lilivyohodhi serikali kupitia mfumokristo.
Ikiwa unataka tuanze upya kujadili hapana neno.
Maalim Faiza kakuwekea picha nadhani umeiona.
Wengi wakubwa wamejaribu kufifilisha historia ya kweli.
Matokeo yake unayajua.
![]()
Cha Waislam kilikuwa AMNUT
Cha Waislam kilikuwa AMNUT
hiki chama kilikuwa na sera ya "uhuru zuia"
na kile cha mtenvu cha ANC
pamoja na na mbinu hizo za uhuru zuia Nyerere alileta uhuru..
Wakati mwingine huwa nafikiria kuwa katika nchi yetu hii kuna watanzania na waislamu,kwa maana ya kwamba waislamu au uislamu ni kama race au nationality nyingine mbali ya utanzania......na kuna watu wanajaribu kuishupalia hii hali ili ionekane kuwa waislamu (na si watanzania) kuwa walifanya jambo fulani au kitu fulani as opposed kwa upande wa pili i.e. ni nadra kusikia wakristo walipigania nchi hii,mimi ninachojua hayo mambo yalikuwa ni collective efforts ya watu wote wakati huo ambao kwa sasa tunawaita watanzania, kipindi hicho walikuwa wanaitwa watanganyika........hii nchi ni ya wote na kila kilichofanyika kilifanywa na watu wote,huu utumwa wa hizi dini tulizoletewa utaisha lini jamani????
Murukulazo,
Ukweli ni kuwa mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa
Tanganyika ni wa pekee.
Wakristo walikuwapo katika harakati hizi lakini lazima ukubali ukweli
kuwahuwezi kufananisha na mchango wa Waislam.
Tangu ilipoasisiwa African Association mwaka wa 1929 Kanisa liliwaonya
waumini wao kutojiingiza katika chama hicho.
Unaweza ukayasoma haya katika, ''Kleist Sykes The Townsman,'' katika
''Modern Tanzanians,'' (Iliffe Ed.) 1973 na aliyeandika habari hizi ni
mjukuu wake Kleist, Daisy Sykes.
Hata TANU ilipoundwa Kanisa lilikuwa halijabadili msimamo wake.
Unaweza kusoma haya katika kitabu changu.
Katika kitabu, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)
The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism,''
(1998) nimeeleza jinsi Nyerere alivyopata shida katika historia hii kiasi
walipoamua kuandika historia ya TANU mara tu baada ya uhuru na mradi
wa kuandika historia hii uliokuwa chini ya Abdul Sykes na Dr. Wilbard
Klerruu ukahujumiwa.
Historia ya TANU ilipokujakuadikwa mwaka wa 1981 na Chuo Cha Kivukoni
ikawa si historia ya TANU bali kitu kingine kabisa.
Wewe hauko peke yako katika kutishika na historia hii ya uhuru na wala
si suala la utumwa wa Uislam kwa wafuasi wake ila ni kuandika historia
kama ilivyokuwa.
Unaweza kusoma zaidi hapa:
Asante sana kwa majibu yako mazuri na kistaarabu tena bila jazba wala mihemko kama ambavyo wengine wangejibu,mkuu kuhusu historia ya TANU na waliokuwepo kipindi hicho,yaani tunazungumzia Dar Es Salaam ya miaka hiyo tokea 1920's hadi kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika,kwa wanaojua historia ya mjii huu watakubaliana na mimi kuwa idadi ya watanganyika waliokuwa wengi ni wale waumini ya dini ya kiislamu kutokana na sababu zilizo wazi na zinazoeleweka kwa sisi wana historia,hivyo basi jambo lolote la wakati huo lazima lingehusisha idadi kubwa ya watu wa imani hiyo kwa namna yoyote ile lakini hili halikuwa suala lao peke yao ilikuwa ni movement nchi nzima iliyokuwa ikiitwa Tanganyika, sasa hofu inakuja hili suala linapogeuzwa kana kwamba lilikuwa ni la waislamu peke yao na si watanganyika,basi kama ni hivyo kulikuwa na kitu nyuma yake kilichojificha ambacho naweza kusema hakikuwa kizuri kwa mustakabali wa nchi yetu,lazima tukubaliane na hili kwanza,kwani kwa kipindi hicho umoja wa kitaifa ndio ulikuwa ni silaha kubwa na nguzo kubwa ya watanganyika kupata uhuru na hatimaye kujitawala,sasa kama linatokea kundi fulani la imani fulani fulani kuteka huo mjadala basi kuna shida kubwa hapo iliyojificha,na ndio maana kwa upande wangu naona suala la kupigania uhuru ndani ya TANU lilikuwa suala la watu wote waliokuwepo hapa Dar es salaam na kwingineko bila kujali itikadi zao,rangi,kabila etc.......naandika haya ili hali nikijua kuwa waafrika tulishagawanywa kwa misingi ya dini za kigeni,waliotutawala na kutuchukua utumwa walihakikisha wanatumia dini zao kufanikisha haya na kutufanya tusiwe wamoja na kwa hakika walifanikiwa hadi leo wamefanikiwa ila mda umefika sasa waafrika tuamke na tuwe kitu kimoja,kama ni nchi ni yetu sote kwa ajili yetu na vizazi vyetu vijavyo..karibu kwa mjadala zaidi natumai kuna mengi ya kujifunza toka pande zote!

Hayo yote uliyosema ni sawa kabisa.
Harakati za uhuru zilikuwa za wananchi wote wa Tanganyika.
Lakini kuna mambo yalimtisha Nyerere baada ya uhuru na hapa ndipo
lilipo tatizo katika utafiti na uandishi wa historia ya uhuru.
Ikiwa umesoma kitabu changu bila shaka utajiuliza, ikiwa hii TANU chanzo
chake ni African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika mbona
hili halipo popote katika historia ya Tanganyika?
Utajiuliza pia iweje Abdul Sykes afanye haya yote katika kumleta Nyerere
katika siasa za ukombozi wa Tanganyika na Nyerere awe kimya kuhusu hili?
Haya ni maswali machache tu ambayo nimetaka uyajue lakini yapo mengi.
Hofu kubwa inayotanda hadi leo ni Uislam.
Walio madarakani wanaiogopa historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika
kwa kuwa imefungamana na Waislam na Uislam.
Ama kuhusu ''dini za kigeni,'' wazee wangu ni Waislam na kwao kama ilivyo
kwetu sisi hatumo katika fikra hiyo ya ''ugeni'' wa Uislam.
Tunamuamini Allah na huu Uislam ndiyo dini aliyotuchaguliwa Mwenyezi Mungu.
Ndiyo maana katika kuupigania uhuru wa Tanganyika kila palipokuwa na ugumu
Waislam walitaka msaada wa Allah.

Asante mkuu kwa chochote tunachoendelea kuelimishana hapa,kwangu mimi sina shida na kuielewa historia ya nchi yetu hasa katika harakati za kudai uhuru toka kwa mkoloni,kwangu mimi history ni matukio yanayoendelea kutokea na kujirudia kila siku aidha kwa namna ile ile au tofauti,hivyo basi tukiliangalia hilo hatuna budi kuweka mbele masilahi ya kitaifa pamoja na umoja wa kitaifa vinginevyo hatutakuwa na taifa imara lenye umoja ulioimarika,kwa upande mwingine ni vigumu kui-suppress history kwa sababu tunajifunza kwa yaliyotokea ili tujue wapi tunakwenda,na kama kuna mahali kuna mtu au watu walijaribu kuiminya history kwa misingi au nia ovu basi hao watakuwa wametenda kosa kubwa katika dunia ya wana-historia.
kuhusu dini bado naamini na najua hizi ni mifumo ya kigeni tu iliyoletwa na wageni kwa sababu mbalimbali zikiwemo kuu za kiuchumi,kitawala,kisiasa......
Asante kwa kujuzana naendelea kusoma kitabu chako.

Nimefurahi tumezungumza.