Azam tv: Kipindi maalum cha sabasaba historia ya kuasisiwa kwa tanu 1954

Iwe mbali kabisa na historia ya TANU au ya NCHI. TANU haikuwa ya WaIslam wala NCHI hii sio ya WaIslam au DINI nyingine yoyote.

WildCard,
Kuhusu TANU kuwa chama kilichokuwa kwa Waislam suala hili tumejadili sana
hapa Majlis halikadhalika jinsi Kanisa lilivyohodhi serikali kupitia mfumokristo.

Ikiwa unataka tuanze upya kujadili hapana neno.
Maalim Faiza kakuwekea picha nadhani umeiona.

Wengi wakubwa wamejaribu kufifilisha historia ya kweli.
Matokeo yake unayajua.

 
Cha Waislam kilikuwa AMNUT
 
Cha Waislam kilikuwa AMNUT

WildCard,
All Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT) kama ilivyokuwa TANU ni
chama kilichoanzishwa na Waislam mwaka 1959.

Waasisi wa AMNUT walikuwa Abdallah Mohamed, Hamisi Hunde, Saleh
Muhsin, Mashado Plantan
na jamaa wengine.

Tofauti kati ya TANU na AMNUT ni kuwa ingawa TANU kilikuwa chama
kilichoanzishwa na Waislam lakini hakikubagua watu wa dini nyingine na kwa
hakika juhudi kubwa zilifanywa na Sheikh Hassan bin Amir kuhakikisha kuwa
TANU inachukua msimamo wa ''nationalist-secularist ideology.''

Nimeeleza haya kwa undani na kwa urefu sana katika kitabu cha Abdul Sykes.

Waislam waliipiga vita AMNUT kwa kuwa kilikuwa chama cha kibaguzi kwa hiyo
hakikustawi.

Congress ya Zuberi Mtemvu haikupinga uhuru ila walitaka Tanganyika iwe ya
Waafrika na huu ulikuwa ubaguzi kwa hiyo chama hicho nacho hakikuweza kuwavutia
wengi.

Ukikisoma kitabu cha Abdul Sykes utajifunza mengi.

Abdul alitaka kumleta Chief David Kidaha Makwaia katika TAA awe rais na kisha
waunde TANU akiwa rais na uhuru ukipatikana awe Waziri Mkuu.

Chief Kidaha ni Mkatoliki.
Hivi ndivyo Abdul alivyomleta Nyerere katika siasa za TAA 1953...the rest is history.

Wazee wetu hawakuwa wabaguzi.
 
hiki chama kilikuwa na sera ya "uhuru zuia"
na kile cha mtenvu cha ANC
pamoja na na mbinu hizo za uhuru zuia Nyerere alileta uhuru..

Leonard Robert,
Hakika AMNUT kilisimama kwenye maslahi ya Waislam katika Tanganyika huru
na kilitaka Waingereza wacheleweshe uhuru hadi pale Waislam watakapokuwa sawa
na Wakristo katika elimu.

Msimamo wa TANU ilikuwa hoja hiyo haina maana yoyote kwa wakati ule kwani
watakaoondoa dhulma si wakoloni bali ni TANU katika Tanganyika huru.

Tanganyika ipate uhuru wake na baada ya hapo ndipo dhulma zote dhidi ya Waislam
zilizoletwa na ukoloni ziondoshwe.

Historia hii nimeieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.
 
Wakati mwingine huwa nafikiria kuwa katika nchi yetu hii kuna watanzania na waislamu,kwa maana ya kwamba waislamu au uislamu ni kama race au nationality nyingine mbali ya utanzania......na kuna watu wanajaribu kuishupalia hii hali ili ionekane kuwa waislamu (na si watanzania) kuwa walifanya jambo fulani au kitu fulani as opposed kwa upande wa pili i.e. ni nadra kusikia wakristo walipigania nchi hii,mimi ninachojua hayo mambo yalikuwa ni collective efforts ya watu wote wakati huo ambao kwa sasa tunawaita watanzania, kipindi hicho walikuwa wanaitwa watanganyika........hii nchi ni ya wote na kila kilichofanyika kilifanywa na watu wote,huu utumwa wa hizi dini tulizoletewa utaisha lini jamani????
 

Murukulazo,
Ukweli ni kuwa mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa
Tanganyika ni wa pekee.

Wakristo walikuwapo katika harakati hizi lakini lazima ukubali ukweli
kuwa huwezi kufananisha na mchango wa Waislam.

Tangu ilipoasisiwa African Association mwaka wa 1929 Kanisa liliwaonya
waumini wao kutojiingiza katika chama hicho.

Unaweza ukayasoma haya katika, ''Kleist Sykes The Townsman,'' katika
''Modern Tanzanians,'' (Iliffe Ed.) 1973 na aliyeandika habari hizi ni
mjukuu wake Kleist, Daisy Sykes.

Hata TANU ilipoundwa Kanisa lilikuwa halijabadili msimamo wake.
Unaweza kusoma haya katika kitabu changu.

Katika kitabu, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)
The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism,''
(1998) nimeeleza jinsi Nyerere alivyopata shida katika historia hii kiasi
walipoamua kuandika historia ya TANU mara tu baada ya uhuru na mradi
wa kuandika historia hii uliokuwa chini ya Abdul Sykes na Dr. Wilbard
Klerruu
ukahujumiwa.

Historia ya TANU ilipokujakuadikwa mwaka wa 1981 na Chuo Cha Kivukoni
ikawa si historia ya TANU bali kitu kingine kabisa.

Wewe hauko peke yako katika kutishika na historia hii ya uhuru na wala
si suala la utumwa wa Uislam kwa wafuasi wake ila ni kuandika historia
kama ilivyokuwa.

Unaweza kusoma zaidi hapa:

http://www.mohammedsaid.com/2015/02/tanzania-country-without-heroes.html
 
 
Wadau anaejua vifurushi vya Azam Tv na bei ya kufunga mzigo mzima wa decorder ukoje naomba anijuze.
Nilipita banda lao pale 7 7 nikakuta watabe wakali wote kwenye tasnia ya habari wako Azam TV. Kumbe Charles Hillary nae kapewa goto refu karudi Bongo kajiweka Azam TV?
Huyu jamaa kaja kuwashika
 
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…