Azam TV kwanini mmeamua kipandisha bei ya ving'amuzi vyenu?

Si juzi tu mlikua mnatoa Hongera tele kwa Azam kutoa mabilioni TFF...au mlidhani hayo mabilioni anayatoa mfukoni mwake?[emoji1787][emoji1787]
 
Si juzi tu mlikua mnatoa Hongera tele kwa Azam kutoa mabilioni TFF...au mlidhani hayo mabilioni anayatoa mfukoni mwake?
Watu tunakimbilia kwakua kina free to air channels kipindi ambacho kifushi kimesha na mfukoni hauko vizuri waeza kumwona hata mama Samia akiongea na TEC
 
Tafuta hela wewe, acha kulia lia Compact ina 49k tu hatafu unalia lia
 
250k ?

Si bora muninyonge
 
Itakua walitaka kupiga,mbona wenyewe wanatangaza bei elekezi ni 145000 dishi, antenna 99000.
plus 65k ya kifurushi, hv kwann walazimishe hyo 65k kuiweka kwenye account yako kifurushi
 
Azam walianza vizuri sana ila sasa nataka nikigawe king'amuzi chao,yaani channels kibao wamezitoa ,hakuna Nigeria movie AMC /Star etc zote wameondoa ,Fox hakuna , Fine living,E! Ent wameondoa yaani full utopolo.
 
Afadhari star time aombe japo kandarasi ya kuchukulia picha kwao ili kuleta ushindani wa kibiashara,washajiona wako peke yao Hamna namna
Tbc nadhani walisema ndo watakuwa na mamlaka ya kuonesha mipira VPL sasa sjui wameshapewa chao
 
Ila sidhani kama walifanya utafiti wa kibiashara. Kuwa na wateja wengi ni uhakika wa fedha nyingi kwa muda mrefu kuliko wateja wachache fedha nyingi kwa muda mchache
 
nafikiri kungekuwa na mdhibiti wa huduma kama hizi aisee, sio wanajipangia wanavyotaka
 
Guys kama kuna mtu anahitaji king'amuzi complete/full kit cha AZAM cha DISH ambacho ni kipya kabisa hakijamaliza hata mwezi na kimeshalipiwa chaneli zote kwa miezi mitatu. naomba anicheki DM tufanye biashara, kinapatikana kwa 165k (non-negotiable price)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…