Azam TV na Bin Zubbery

Azam TV na Bin Zubbery

balibabambonahi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Posts
15,771
Reaction score
14,294
Hivi kwa kuanzisha kipindi hiki cha kila Jumapili asubuhi na hivi ninavyoandika kinaendelea mlikuwa na lengo gani? Bin Zubbery mwenyewe na wageni wake wako biased dhidi ya timu ya Yanga.

Wanaponda kila zuri la Yanga na inaonekana kama lengo ni kuikatisha tamaa Yanga na kuwakatisha tamaa wafuasi, mashabiki na wanachama wa Yanga.

Akialikwa mchezaji wa zamani mfano leo, alikuwa Omary Tamba ambaye alicheza Simba lakini aliposema kwao wote ni Yanga pamoja na yeye mwenyewe, Bin Zubbery kakunja sura na kuonesha hajapenda.

Basi kipindi kiitwe cha Simba na hao wengine kuliko kukiita Sports wakati kiko biased. Kwanini bin Zubbery asiwe impartial? Shida iko wapi? Nina wasiwasi pia na weledi wa bin Zubbery maana wakati anaongelea kuhusu baraza jipya la mawaziri, anatoa taarifa kana kwamba baraza limetangazwa leo asubuhi bila kujua kwamba, kwa dunia ya leo yenye mapinduzi ya teknolojia ya habari, habari ya jana jioni siyo habari tena.

Angejikita katika uchambuzi wa baraza na walioteuliwa siyo kuanza kusoma majina, hata hivyo hata majina yenyewe anayasoma kwa taabu sana. Nimeshangaa Sana.
 
Hao ndo akina Ahmed Ally waliokua wanajificha kweny kichaka cha utangazaji kumbe wana mahaba na timu flani.

Watangazaji wa michongo hao. Wanalipwa na wanatumika kuichafua Yanga. Na sisi tunasema watashindwa.
 
Vipi kwa wacha mbuzi wenu wanaoichafua simba na Mo kila kukicha juu ya uwekezaji na ujenzi wa uwanja wa Bunju? Wacha Mbuzi wenu nawaasa bora wawe wacha Mungu kama wameshindwa kuzungumzia ubora na mafanikio ya Simba CAF na Ligi Kuu la Tanzania. Wacha Mbuzi wengi wa Tanzania ni kama marefarii wetu tu wanaona micro aila macra hawaoni yaani wao ni zaidi ya VAR. Hivi kweli Feisal alifanyiwa faulo hadi refa aliweka penalt dhidi ya Namungo? Kila mechi ya Yanga lazima refa awe Man of the match ni upuuzi tu.
 
Uovu mmoja hauhalalishi uovu mwingine,kama una hoja yako kuhusu hicho unachokisema,anzisha Uzi kuhusu hilo.Maisha ya Leo hayaendani na sheria ya JICHO kwa JICHO ama jino kwa jino.
 
Labda kama Mwandishi humjui Mohammed Zubeiry

Sie tunayemfahamu toka miaka ya 90 akiandikia gazeti la DIMBA kisha gazeti dada la BINGWA na akiendesha blog yake ya binzubeiry ambayo kwa sasa inatumia anuani ya binzubeiry.co.tz tunajua kuwa huyu jamaa ni Yanga lia lia lia. Kusema anaichukia Yanga labda kama anasema kitu ambacho wewe hujakipenda kwa kuwa ni ukweli lakini kuhusu mapenzi ni Yanga mno mno mno

Uliza na fuatilia ujue
 
Japokuwa mimi Simba damu, ila ukweli usemwe bhana, huyo bin zubery ni mnyama lia lia, nilidhani ni mimi peke yangu nimeliona hilo kumbe tupo wengi [emoji23][emoji23] .. all in all sio dhambi ila ajitahidi kubalance mapenzi yake binafsi na kazi kwa mustakabali mzuri wa kazi yake.
 
Tangu lini bin zubery amekuwa shabiki wa Simba? Ni Yanga wa kutupwa huyo
 
Huyo jamaa pamoja na kuwa mwandishi wa habari za michezo wa muda mrefu, huwa namuona kama hamna kitu, kuna wakati huwa anajipachika kazi ya uchambuzi, unaona kabisa anaongea vitu illogical
 
Tangu lini bin zubery amekuwa shabiki wa Simba? Ni Yanga wa kutupwa huyo
Achana na ushabiki wake binafsi,tuongelee anavyoendesha kipindi.Ndo maana nikauliza malengo ya kipindi.Bin Zubbery awezo kuwa Yanga Lia Lia kama unavyodai lakini akalazimika kufuata matakwa ya aliyemwajiri.Kumbuka amlipaye mpiga zumari ndiye huamua apige mziki gani.Tujadili jinsi kipindi kinavyoendeshwa.Mimi sijalalamika kwamba Bin Zubbery ni Simba ama Yanga nimeongelea jinsi kipindi kinavyoendeshwa.
 
Tukimaliza bin zubery tuje kwa manara ni shabiki wa timu gani, afate mama, afate bakhresa, afate job, wafate watu maarufu wote.
Hapa topic siyo nani ni nani bali ni jinsi kipindi kinavyoendeshwa with prejudice vs Yanga.
 
Achana na ushabiki wake binafsi,tuongelee anavyoendesha kipindi.Ndo maana nikauliza malengo ya kipindi.Bin Zubbery awezo kuwa Yanga Lia Lia kama unavyodai lakini akalazimika kufuata matakwa ya aliyemwajiri.Kumbuka amlipaye mpiga zumari ndiye huamua apige mziki gani.Tujadili jinai kipindi kinavyoendeshwa.Mimi sijalalamika kwamba Bin Zubbery ni Simba ama Yanga nimeongelea jinai kipindi kinavyoendeshwa.
Hicho kipindi sijawahi kukiona, maana sijawahi kuwa na mahaba na king'amuzi cha Azam. Mimi nimezungumza ninavyomfahamu miaka mingi.
 
Kipindi kiisha kuna majina yanapanda, sijui cameraman, director, producer etc. Yeye ni host tu anaambiwa afanyeje.
Ikiwa lengo ni kuipondea yanga ataambiwa afanye ivo au simba vilevile.
Usichukulie serious sana haya mambo ya media lengo ni kuchukua attention yako, ili wapige pesa.
 
Hao ndo akina Ahmed Ally waliokua wanajificha kweny kichaka cha utangazaji kumbe wana mahaba na timu flani.

Watangazaji wa michongo hao. Wanalipwa na wanatumika kuichafua Yanga. Na sisi tunasema watashindwa.
Baba mkwe Simba team kubwa
 
Kipindi ni kizuri sana, binafsi naenjoy,,, Bin Zubeiry ni mtu wa utani utani sana anaweza akapiga dongo Simba au Yanga so chukulia kipindi kama burudani utaenjoy vyema.
Style yake ya ucheshi ucheshi naifananisha na Alex Luambano wa Clouds

Pamoja na yote lakini kipindi hiki cha Sports AM ni bonge la moja la kipindi hasa umkute Mchambuzi Ramadhan Mbwaduke utafurahi sana, japo zamani alikuwepo pía Jemedari Said kabla hajatimkia EFM

Moja ya interview iliyonivutia sana ni siku walipomkaribisha legend wa riadha Sulemani Nyambui.
Nyambui ni mtu mmoja mcheshi, muwazi pamoja na umri kumkimbia lakn ana kumbukumbu ya mambo mengi sana ya matukio ktk enzi zake

Interview ilikuwa tamu sana mpaka ikapelekea kuiweka ktk session ya weekend iliyofuata
 
Hivi kwa kuanzisha kipindi hiki cha kila Jumapili asubuhi na hivi ninavyoandika kinaendelea mlikuwa na lengo gani? Bin Zubbery mwenyewe na wageni wake wako biased dhidi ya timu ya Yanga.

Wanaponda kila zuri la Yanga na inaonekana kama lengo ni kuikatisha tamaa Yanga na kuwakatisha tamaa wafuasi, mashabiki na wanachama wa Yanga.

Akialikwa mchezaji wa zamani mfano leo, alikuwa Omary Tamba ambaye alicheza Simba lakini aliposema kwao wote ni Yanga pamoja na yeye mwenyewe, Bin Zubbery kakunja sura na kuonesha hajapenda.

Basi kipindi kiitwe cha Simba na hao wengine kuliko kukiita Sports wakati kiko biased. Kwanini bin Zubbery asiwe impartial? Shida iko wapi? Nina wasiwasi pia na weledi wa bin Zubbery maana wakati anaongelea kuhusu baraza jipya la mawaziri, anatoa taarifa kana kwamba baraza limetangazwa leo asubuhi bila kujua kwamba, kwa dunia ya leo yenye mapinduzi ya teknolojia ya habari, habari ya jana jioni siyo habari tena.

Angejikita katika uchambuzi wa baraza na walioteuliwa siyo kuanza kusoma majina, hata hivyo hata majina yenyewe anayasoma kwa taabu sana. Nimeshangaa Sana.
Hakuna tv,redio au magazeti yanayoweza kuififisha yanga

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom