The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mahakama Kuu ya Tanzania imeipa ushindi Azam Media dhidi ya Bondia, Amos Mwamakula aliyetakiwa kulipwa fidia ya Tsh. milioni 250 baada ya kushinda kesi ya uvunjifu wa haki miliki ya wazo lake ambayo ilitolewa na Mahakama ya Kivukoni.
Ushindi huo wa Azam unakuja baada ya kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa August 22, 2024 na Mahakama ya Kivukoni inayoketi Kinondoni ambayo iliamuru Mwamakula alipwe fidia hiyo baada ya Azam kutumia wazo lake la Boxing Kazi Kazi na kuitwa vitasa.
Hukumu ya rufani hiyo namba 28052 ya mwaka 2024, imetolewa leo ambapo tumezungumza na Wakili Neema Mbaga anayeiwakilisha Azam ambapo amesema
“Siku ya leo tunafuraha sana tunamshukuru Mungu hukumu imesomwa mbele ya Mahakama Kuu na tumeshinda kesi, yale maamuzi ya Mahakama ya chini yametupiliwa mbali, Mahakama hii kuu imeona kuwa sio sahihi kwamba kipindi cha Boxing Kazi Kazi kina mfanano na amedadavua kuhusu hati miliki na nini kinacholindwa, na kwamba kinacholindwa ni ubunfiu wa Mtu ama uandaaji”