Azam TV yatangaza kuanza mazungumzo EPL na La Liga

Azam TV yatangaza kuanza mazungumzo EPL na La Liga

KIBEHA

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
259
Reaction score
128
Watanzania tukae mkao wa kula.

Jana usiku mkombozi wa Afrika Mashariki, AZAM TV, ilitangaza kuanza mazungumzo kwa ajili ya kuonyesha EPL na LA LIGA moja kwa moja kuja majumbani kwetu yani live bila zengwe.

Ombi langu kwa Azam TV na UEFA; msitusahau tumenyanyasika sana.

Bravo sana Bakhresa!

=================
=================

Mambo yakienda vizuri, Azam TV itakuwa kituo cha kwanza cha runinga nchini kurusha ‘live' mechi za Ligi Kuu England kwa Lugha ya Kiswahili.

Hadi sasa uongozi wa Azam TV upo kwenye mipango ya kuhakikisha unarusha ligi hiyo live kutoka England katika msimu ujao unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando, alisema wamejipanga kuhakikisha wanalikamilisha hilo mapema.

"Tunafanya juhudi kubwa ili tulifanikishe hilo mapema, ila wahusika ndiyo wenye uamuzi wa mwisho katika kutupa haki ya matangazo hayo, tumedhamiria pia kuonyesha Ligi ya Hispania.

"Wakati tukipanga haya, tuna nia ya kuboresha muonekano wa ligi yetu ya Tanzania (Ligi Kuu Bara) msimu ujao ambapo tunataka ionekane katika ubora wa hali ya juu zaidi," alisema Tido.

Katika hatua nyingine, Tido alisema katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi hadi utakapofanyika, watakuwa wakiwaletea watazamaji wao matangazo ya matukio mengi kuhusu uchaguzi huo.

Chanzo: SalehJembe
 
Kama itakuwa kweli itakuwa powaaa saana.
Dstv hatar sana.
 
Nimeshanunua ki-azam changu hapa, ntakilipia pindi watakapoweka ligi hizo tajwa hapo juu
 
mkuu kingamuzi cha azam kuanzia mwezi wa huu kukinunua ni zaid ya laki mbil. kwa hiyo hamna tofaut na dstv..sasa ya nn nichukue azam yenye chanel nying zszokuwa na tija.niache dstv ambayo ni world wide?...na channel over the world
 
Wewe umetumwa na startimes
 
mkuu kingamuzi cha azam kuanzia mwezi wa huu kukinunua ni zaid ya laki mbil. kwa hiyo hamna tofaut na dstv..sasa ya nn nichukue azam yenye chanel nying zszokuwa na tija.niache dstv ambayo ni world wide?...na channel over the world

Mkuu hiyo si initial cost ya installation,,lakini gharama ya subscription ipo chini sana ...kwenye subscription fee ndipo DSTV inapokuwa juu kupita kiasi..
 
mkuu kingamuzi cha azam kuanzia mwezi wa huu kukinunua ni zaid ya laki mbil. kwa hiyo hamna tofaut na dstv..sasa ya nn nichukue azam yenye chanel nying zszokuwa na tija.niache dstv ambayo ni world wide?...na channel over the world

Huo ni ukweli mtupu,na azam hawezi nunua mechi zote,zaidi atanunua mechi moja kwa wiki na ambazo wao watampangia.
 
Huo ni ukweli mtupu,na azam hawezi nunua mechi zote,zaidi atanunua mechi moja kwa wiki na ambazo wao watampangia.

huo ndio ukwel mkuu.halafu azam atakuwa anajiangaisha tu kwa kuwa Dstv sio mmliki wa barclays.laliga.au bundesliga...mfano wenye haki ya kurusha barclays ni Skysport hawa kina Dstv.kwa africa tena sio nch zote
dstv hawez akubal et awaache wateja wa east africa kisa azamtv..bora dstv wapunguze garama na sio kitu kingine
 
da kwa eafa waache kwanza msimu huu utakao anza upite maana duuuuuu tutatokaje night maana tulisha jizoelea kuaga twaenda kutazana mech?
 
Last month, the Federal Government decided to break the monopoly of Digital Satellite Television (DSTV) over the broadcast of some programmes in the country, notably the English Premiership League (EPL).

And now, the management of EPL has separated Nigeria from the rest of Africa in its marketing deals, thereby removing the nation from the grip of Multichoice, owners of DSTV. This has set the stage for a healthier competition in the local media market.

This is a major departure from the past. That it took so long to deregulate the DSTV monopoly is shocking. Despite the near-cult
following of English football in many parts of Africa, with the potential of willing and capable investors, Multichoice had secured the exclusive rights, on behalf of all African countries, to transmit EPL and channels like Discovery, Reality TV, National Geographic to the continent.

And to ensure that it remains the only advantageous satellite subscription company in Africa, it has used, over the years, its enormous resources to negotiate for foreign programmes, on the pretext of doing so for the good of the continent.

But while it is wrong to question the right of Multichoice to strengthen its profit base, the tendency of the South African company to stifle competition and maintain its stranglehold on the broadcast industry in Africa amounts to unfair trade practice.

The EPL gesture will enhance Nigeria's quest for social and economic status as the country now own the rights to air EPL matches via satellite. Not only that, domestic free-to-air television organisations have also been permitted to broadcast two games every week freely.

In addition to liberalising the choices of Nigerians, these are, no doubt, remarkable contributions to the growth of soccer in the country. And if EPL's plan to invest in a Nigerian television station is actualised, the local football league that has wallowed in mediocrity for long will receive a big boost. But before then, both sporting and media stakeholders need to maximise EPL's offer.

The effort of the Federal Ministry of Information and National Orientation in facilitating this breakthrough is commendable. Its directive to the Nigerian Broadcasting Commission (NBC) to inform the managers of EPL of government's resolution is directly responsible for the concession.

The minister, Mr. Frank Nweke, represented the mood of the nation in London on September 4 when he declared: "Nigeria would do anything within its power to ensure that its local businesses are protected ... you will all understand that any
government that fails to protect its local economy is not worth being called a government."

That pronouncement should not stop at mere rhetoric. Rather, it should be taken as a self-imposed marching
order. The task of creating the environment for proper private sector participation is the government's.

That means the infrastructure and policy framework that would enable the new licensee to attain and possibly surpass DSTV's achievements should be put in place.

And for the local business community, this is one opportunity to justify the EPL management's confidence in Nigeria's capacity to
perform.

Source: balancing act
 
Mambo yakienda vizuri, Azam TV itakuwa kituo cha kwanza cha runinga nchini kurusha ‘live' mechi za Ligi Kuu England kwa Lugha ya Kiswahili.

Hadi sasa uongozi wa Azam TV upo kwenye mipango ya kuhakikisha unarusha ligi hiyo live kutoka England katika msimu ujao unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando, alisema wamejipanga kuhakikisha wanalikamilisha hilo mapema.

"Tunafanya juhudi kubwa ili tulifanikishe hilo mapema, ila wahusika ndiyo wenye uamuzi wa mwisho katika kutupa haki ya matangazo hayo, tumedhamiria pia kuonyesha Ligi ya Hispania.

"Wakati tukipanga haya, tuna nia ya kuboresha muonekano wa ligi yetu ya Tanzania (Ligi Kuu Bara) msimu ujao ambapo tunataka ionekane katika ubora wa hali ya juu zaidi," alisema Tido.

Katika hatua nyingine, Tido alisema katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi hadi utakapofanyika, watakuwa wakiwaletea watazamaji wao matangazo ya matukio mengi kuhusu uchaguzi huo.

Chanzo: SalehJembe
 
Jamani nijuavyo tayari Dstv kashinda haki ya kuonesha EPL kwa misimu mitatu kuanzia msimu huu, hadi baada ya miaka mitati ndo tenda zitatolewa tena
 
Back
Top Bottom