Azam wameamua kuwa wahuni kama kaka zao sasa ligi kuu itanoga

Azam wameamua kuwa wahuni kama kaka zao sasa ligi kuu itanoga

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Kalimangonga Ongara ni mtoto wa mjini,tangu aichukue timu kuna mabadiliko nayaona.

Timu imeamua kuwa ya kihuni kama wahuni wa jangwani na msimbazi.

Azam sasa kuna viashiria vya kununua mechi kama wanajangwani
Azam sasa kuna viashiria vya ndumba kama msimbazi
Azam sasa wanafanya uhuni kwenye usajili kwa kupora wachezaji kibabe kama wenzao

Huu ni uhuni mzuri sana unaleta ushindani kwenye mpira wetu.

Nilishangaa Qatar walivyotaka kutenganisha mpira na uhuni.
Miaka yote Azam olikuwa inafeli hapa.

Simba inafeli sasa sio sababu ya Mo wala nani bali Hans Pope

Nani hajui ubabe wake,aliwahi kuwachana live Chama na Kapombe walipocheza chini ya kiwango,Simba ya sasa hakuna mtu anaweza kumchana Chama

Chini ya Hans Poppe Aziz ki ,Adebayo na Manzoki wangekuwa Simba.

Mpira ni mchezo wa kihuni
Tutarajie ushindani na ligi bora
 
Hawez kuwafikia kulwa na Doto wale wapo mbali sana,kibaya zaidi watendaji wa azam wana DNA za hizi timu mbili kuna muda wanafanya vigisu lakin wanakwama
Sasa ni kama wamestuka kama mbwai mbwai tu,
Timu ikikuwa ikitaka kuroga viongozi wanasema Mtume SAW kakataza shirki.timu ikitaka kuhonga waamuzi wanasema ni dhambi na kosa kisheria.
Ni kama Kalimangonga amewaamsha
 
Azam kinachowaangusha ni kukosa fanbase kubwa kama Simba na Yanga

Mashabiki hawachezi ila mashabiki ndio hutia presha kwa wachezaji kujituma zaidi
Mashabiki ndio hutia presha kwa waamuzi kutoa maamuzi magumu dhidi ya timu yao kwenye mechi, yaani waamuzi kupendelea, na viongozi kusajili kibabe
Mashabiki hutia sana ari kwa timu

Utashangaa sana Azam pamoja na kuwa ipo Dar inazidiwa mauzo ya tiketi na timu kama Biashara United
Kwa hali hiyo kuzifikia klabu za Kariakoo ni ngumu
 
Hata wafanyeje! Wasahau kuhusu ubingwa. Wataishia tu kugombania nafasi ya 2 na ile ya 3, na kaka yake Ngada Fc.
Umeongea kishabiki, natamani kuiona Azam ikiwatikisa kulwa na doto ligi itanogaio kila siku simba yanga,simba yanga.
 
Umeongea kishabiki, natamani kuiona Azam ikiwatikisa kulwa na doto ligi itanogaio kila siku simba yanga,simba yanga.
Azam uwezo huo Hana. Ameshindwa kushawishi watu kumpenda Kwa sababu alianzisha timu kama ya kifamilia. Azam anazidiwa mashabiki hata na KMC Kwa vijana wa Kindondoni. Unaowaona uwanjani ni aidha Wafanyakazi, waliolipwa au wachache waliochukizwa na Jambo Fulani huko Kulwa na Dotto. Kwenda uwanjani Peke yako kama mchawi ni ngumu kushinda maana Hakuna anayekupa hamasa. Yaani ukishindwa wanaoudhika ni wachache na ukishinda wanaofurahi ni wachache pia.
 
Azam anaweza kuwateka waru wa mbagala yote akiamua,na mbagala ina watu,mfano akafadhili timu zote za mbagala kwa kugawa jezi na mipira,akagawa jezi na mipira kwa shuke zote za mbagala wanafunzi wote wataishabikia,miaka mitano tu yuko mbali na fanbase kubwa
 
Tatizo utopolo mnadhani mpira ni mapenzi ama mchezo wa kuigiza.

Mpira ni ajira na wachezaji wapo kazini.Msiwalazimishe kuwa mashabiki.Hayo ni maisha yao.

Asante wakili msomi kwenda kuwaamsha.Wewe unachukua 18M kwa nini Fei alipwe 4M?
Hawa viongozi wa utopolo ni matapeli mjue

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom