Azam yamrejesha kikosini mwalimu Stewart Hall

Azam yamrejesha kikosini mwalimu Stewart Hall

Mbilimbi Mbovu

Senior Member
Joined
May 25, 2015
Posts
185
Reaction score
119
Taarifa hii imetolewa na mwanahabari Omari Katanga kupitia ukurasa wake wa Facebook, pengine kwenye kipindi cha michezo cha EFM tutapata taarifa kwa kina.

Kwa sasa habari iliyopo ndio hiyo!

==============================
==============================


‘Baada ya muda mrefu wa fununu, Azam wamekata kiu leo na kuanika makocha wao wapya wanaotoka Uingereza.'

HII KUFURU! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya jana uongozi wa Azam FC kumtangaza Muingereza Stewart John Hall kuwa kocha mkuu mpya akisaidia na makocha kutoka klabu kubwa za soka ulimwenguni ikiwamo Arsenal ya Ligi Kuu ya England (EPL).

Baada ya muda mrefu wa kusubiri kitakachojiri, uongozi wa Azam kupitia kwa msemaji wake, Jaffar Idd Maganga, leo umetangaza kumrejesha Hall na mabadiliko mengine makubwa katika benchi la ufundi.

Maganga amesema kuwa Hall aliyewahi kuinoa Azam FC na kuipa mafanikio makubwa ukiwamo ubingwa wa msimu wa 2013/14 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (ingawa aliishia mzunguko wa pili na kumpisha Mcameroon Joseph Omog), amepewa mkataba wa miaka miwili na atakuwa akisaidiwa na Mganda George ‘Best' Nsimbe.

"Kuna ongezeko na punguzo katika benchi la ufundi na idara ya utawala na fedha kutokana na uamuzi uliofanywa na uongozi wa Azam FC leo (jana)," amesema.

Mark Philip raia wa Uingereza aliyewahi kufanya kazi katika klabu ya Bolton Wanderers ya Uingereza na kituo cha kulea vijana wenye vipaji (Academy) cha klabu ya Aston Villa ya Uingereza pia, anakuwa kocha wa makipa wa Azam akisaidiwa na mzawa Idd Abubakar.

Philip mwenye leseni A ya UEFA katika ukocha, amepewa mkataba wa miaka miwili na matajiri hao wa Tanzania.

Aidha, Mromania Mario Mariana ameajiriwa kuwa kocha wa timu ya vijana ya Azam na atasaidiwa na wazawa Dennis Kitambi (aliyekuwa kocha mkuu wa Ndanda FC msimu uliopita kabla ya kutimkia Azam) na Idd Cheche.

Mariana mwenye leseni ya UEFA Pro katika ukocha, pia atakuwa akiionoa timu ya Azam ya wakubwa akiwa kocha wa viungo (Physical Fitness).

Katika idara ya utawala na fedha uongozi wa Azam FC umemwajiri Muingereza mwingine, El Bankya kuwa meneja wa idara hiyo.

Muingereza huyo mwenye asili ya Uganda aliyewahi kufanya kazi katika klabu za Arsenal na Southampton za EPL, amepewa mkataba wa miaka miwili pia.

"Waajiriwa wote wapya wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam Juni 8 na tutaanza rasmi kambi ya michuano ya Kombe la Kagame Juni 15 hapa Dar es Salaam," amesema zaidi Maganga.


Chanzo: ShafihDauda.com
 
Huyu mzungu anakuwa kama tiara mara aondoke mara arudishwe
 
Huyu mzungu anakuwa kama tiara mara aondoke mara arudishwe
Wana mihemko nae, wanamfukuza na kumrudisha... Mara ya mwisho nilisikia alikuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Soka cha Kidongo Chekundu kinachojengwa kwa ushirikiano wa Serikali, Klabu ya Sunderland na Shirika la Umeme la Symbion!
 
Huyu mzungu anakuwa kama tiara mara aondoke mara arudishwe
Azam wanacheza ngoma ya wenzao Simba na Yanga, hawajui kama viongozi wa upande ule wapo kama hawapo, wapige magumashi yao kisha wakagombee ubunge!
 
Back
Top Bottom