Atukuzwaye
Senior Member
- Oct 5, 2026
- 191
- 250
Mkazi wa Kijiji cha Mafisa, Kata ya Mvungwe, Wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga, Juma Hamisi Msilagi (69), amezawadiwa shilingi elfu ishirini baada ya kusalimisha kwa hiari silaha moja aina ya gobore aliyokuwa akiimiliki kinyume cha Sheria.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Tanzania, Msilagi amechukua hatua hiyo kufuatia wito wa kusalimisha silaha zinazomilikiwa kinyume cha Sheria uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi. Baada ya kusalimisha silaha hiyo, Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kilindi, ASP Mtera amemkabidhi shilingi 20,000 kama zawadi na njia ya kuhamasisha Wananchi wengine wenye silaha haramu kujitokeza na kuzisalimisha kwa hiari.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi zake za kuhamasisha Wananchi kuitikia wito wa msamaha wa kusalimisha silaha zinazomilikiwa kinyume cha Sheria, kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama katika Jamii.
Jamani mkisalimisha hayo magobore tunakikisha jamii salama lakini pia unaweza ukajipatia ka buku twenti ka soda kama babu hapo😀😀