Azim Dewji: Mbunge akiwatumikia wananchi hatajiriki bali anafilisika

Azim Dewji: Mbunge akiwatumikia wananchi hatajiriki bali anafilisika

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251

Charles William Mara nyingi ninapotoka kuzungumzia kuhusu masuala ya amani, utulivu, na jinsi ambavyo watu hawatakiwi kuendeshwa na propaganda, kuna watu wamekuwa wakisema Mzee Azim Dewji anatakiwa kuungana na Watanzania ambao wanalaani baadhi ya vitu vinavyotokea hapa Tanzania.

Matukio kama ya utekaji na kadhalika, kwa sababu yeye mwenyewe liliwahi kutokea kwenye familia yake; kijana wake Mo Dewji alitekwa, na Watanzania waliunganisha nguvu kudai Mo arejee. Lakini yanapotokea matukio mengine ya utekaji, Azim Dewji anakaa kama upande wa kuitetea serikali.

Mzee Azim Dewji: Si kweli. Jambo lolote linalotokea baya mimi nasema, na wala simwogopi mtu. Unaona? Na unatakiwa uwe hivyo. Kwamba kukiwa mtu anastahili sifa, mpe sifa yake. Kama mtu anastahili kuambiwa, mwambie. Sisi kijini vile vile tunaambiwa kuna kitu kinaitwa Amr bil Ma'ruf — kwamba mtu anapokosea, ni wajibu, ni agizo la Mungu kumkosoa. Kwa hiyo jambo linapoharibika, lazima tunasema.

Charles William: Baadhi labda waliumia kidogo uliposema wakati ule kwamba hauamini kama Humphrey Polepole ametekwa. Kwa hiyo wakaona badala ya kuungana na familia ambayo inatfuta ni wapi alipo, wewe umeenda kutoa kauli ambayo imeonekana kama ni dhihaki.

Mzee Azim Dewji: Si kweli. Kwa mtazamo wangu—kila mtu si ana haki ya kuwa na mtazamo wake bwana? Wewe una haki ya kuwa na mtazamo wako, na ule ni mtazamo wangu. Mimi sio kiongozi wa serikali wala sio kiongozi wa chama; mimi ni mwanachama tu. Unaona? Unapokuja kuzungumza maneno ambayo hayatambuliki, basi inakuwa kwamba au umetumwa au wewe una sababu nyingine. Unaona? Kwamba unaanza kusema kuwa kuna kipindi kimoja...

Charles William: Anasema bwana Rais anapoenda nyumbani, mlinzi wake anajua mlango ni huu na unamwambia hapa, akifika anafungua...

Mzee Azim Dewji: Lakini hiyo ni kawaida mahali popote. Ukimwangalia rais yeyote ambapo unapoenda, anaambiwa hivyo: kwamba "Hii gari ni hii hapa" — kwani Rais haoni gari? Au kama kuna mahali pa kutoka, haonyeshwi? Sasa hizo ni protokali za kila mahali. Lakini unapoanza kuleta maneno ambayo hatuyaelewi, lazima tutakufikiria tu vinginevyo — au umetumwa, au una ajenda gani. Unaona? Kwa hiyo mimi nasema Polepole namheshimu, Lissu ni ndugu yangu mimi sina shida naye, lakini tunatakiwa tuwe tunaweka uzalendo wetu mbele.

Charles William: Kwa mtazamo wako kuhusu swala la mambo ya watu kupotea na utekaji?

Mzee Azim Dewji:Kama mtu kupotea kweli si kitu kizuri kabisa. Kama wanapotezwa na serikali au wanapotezwa na chama—na mimi siamini kwamba serikali inaweza kuwa na sababu ya kumpoteza mtu. Sioni. Kuna vitu vingi tu mtu anaweza akafungua, anaweza akataftiwa kesi tu akamwondoa kwenye reli. Kwa nini amwue? Hakuna sababu ya kumwua.

Pia soma: Azim Dewji: Siamini serikali inaweza kuwa na sababu ya kumpoteza mtu; anaweza kufungwa au kutafutiwa kesi ili kumuondoa kwenye reli
 
Back
Top Bottom