Azim Dewji: Nilimkataa Robertinho kuwa Kocha wa Simba

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
22,719
Reaction score
40,739
"Niliwauliza viongozi wa Simba Sc huyu kocha ametoka timu gani wakaniambia ametoka Vipers ya Uganda, niliwaambia mbona Vipers ni timu ndogo sana sisi tunataka kocha mkubwa sio kocha wa kutoka kwenye timu ndogo sisi malengo yetu ni makubwa”

Azim Dewji - Mfadhili wa Zamani wa Simba na mdau wa soka nchini akizungumza sakata la kocha Roberto Oliveira kutimuliwa.
 
Azam TV na Moto wao!!
 
Kutoka timu ndogo si tatizo, wapo makocha waliotoka timu ndogo na bado wakawa na uwezo, shida tu kwa soka lake lile hakuwa kocha mzuri kwetu, ameonesha uwezo mdogo kuliko aliouonesha vipers.
Kweli mkuu. Suala ni kutafuta kocha bora anaendana na aina ya timu iliyonayo wala si kutoka timu kubwa wala ndogo.

Unaweza kuchukua kocha kutoka timu kubwa lakini kumbe ana uwezo wa kawaida tu(waswahili husema anatembelea nyota) ukampa timu yenye wachezaji wa kawaida akaishia kuunderperform.

Vilevile unaweza kuchukua kocha mwenye uwezo kutoka timu ndogo ukampa wachezaji wazuri wenye uwezo kuliko timu ndogo aliyotoka na akafanya vizuri zaidi ya mategemeo. So suala la msingi ni kutafuta kocha bora bila kujali anatoka timu gani iwe kubwa au ndogo.
 
Kumbe matajiri ni Wajinga pia?

Amesoma hata CV ya robertinho kweli?

Team Alizofundisha mbona ni kubwa kuliko simba.

HIvi Fluminese na Simba ipi ni team kubwa?

Sven anavyokuja Simba alikuwa amewahi fundisha Club yoyote?
Hana ujinga na yuko sahihi. Labda wewe ndo una ujinga.

Wadau wengi wa Simba walikuwa wanataka aje kocha aliyewahi kupata mafanikio makubwa kwenye soka la Africa (CAFCL au CAFCC). Robertinho ana CV gani kubwa kwenye hayo mashindano?

Wanasimba walitaka uongozi usilete tena hawa makocha wa kizungu wasiolijua vyema soka la Afrika (wakiwemo Sven Vandernbrock, Robertinho,n.k) bali waletwe wababe wa Kiafrika kama akina Florent Ibenge,aliyekuwa kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya Ghana,n.k. Haya huyo Robertinho anafikia CV ya hao niliowataja?

Credit haikuwa kufundisha Fluminense, maana kuna mtu alikuwa kutoka Real Madrid (Gomez) na bado akachemka.Credit ilikuwa kulijua na kuliweza soka la Africa.
 
Tatizo ni kuropoka kwingi as if mtaweza kuwalipa, msidhani kupata kocha mwenye mafanikio ya kimataifa mtakuwa mnamlipa pesa ya madafu, inahitajika hela kweli

Jaribu kufuatilia wenzetu wa Afrika Kaskazini ama Kusini wanawapipa sh ngapi ndio utajua kuwa, viongozi na mashabiki kinachowaponza ni kuropoka ilhali kugharamia hawawezi
 
Sawa, nimekuelewa wewe unayegharamia usajili wa wachezaji na kuleta makocha klabuni kwako.
 
I

Issue ni muache soka la Simba na Yanga, kuna mengi nje ya utani wa jadi, haiwezekani mdai kocha hana viwango na mmeanza nae ligi

Ingekuwa sivyo, mngemtoa kabla ya kuanza michuano
 
Back
Top Bottom