mada nyingi za bwana william huwa hazina mwisho,yaani ni duara nikimaanisha mtakuwa mnakwenda na kuzunguka na kurudia rudia kile mlichokisema mwanzo
na yeye atasisitiza na majibu yake ya AZIMIO LA ARUSHA HALIKUWA NA TIJA x1000000
kwake yeye hakuna hata mahala penye unafuu hususani AZIMIO LA ARUSHA
na bado william ana amini kuwa hata ufisadi wa leo,kutokuwajibika kwa viongozi,kujilimbikizia mali yote hayo ni zao la AZIMIO LA ARUSHA
Migomo ya wanafunzi,madaktari,mauaji migodini,mirahaba midogo na mikataba feki mogodini bado kaka yangu William anaona ni kosa la AZIMIO LA ARUSHA
gape la wenye nacho na wasionacho,matatizo ya umeme,maji na madawa hosptalini,kudolola kwa uchumi yote hayo yanamfanya william Kulichukia AZIMIO LA ARUSHA
kuuzwa kwa nyumba za serikali zilizojengwa kwa AZIMIO LA ARUSHA, baadhi ya njia za reli kuto kufanya kazi,viwanda kufa,msongamano wa magari na watu DSM kaka William anatupa lawama kwa AZIMIO LA ARUSHA
sijui na bado siamini kama kweli william malecela anaelewa vyema AZIMIO LA ARUSHA kwa nini lilianzishwa,malengo na majukumu ya azimio la arusha
sijaona hata sehemu ambapo william ametueleza faida ya AZIMIO LA ZANZIBAR labda hajui kama lipo na linafanya kazi,ama malengo ya AZIMIO LA ZANZIBAR yanamfurahisha ndio maana haliongelei wala hataki kuligusa
lakini kiukweli AZIMIO LA ARUSHA limefanya makubwa sana ukifananisha na AZIMIO LA ZANZIBAR lililokuja na meno ya kuila nchi na wanyonge kupata tabu kama watumwa ndani ya nchi yao