Alright
Waberoya.
Naomba niwaulize swali wewe na
W. J. Malecela. Hivi sheria uandaliwa na kutungwa ili ku-enforce mambo gani? Je, utungwa ku-enforce abstract things?
Mimi naelewa kwamba, sheria utungwa katika kuweza ku-enforce misingi fulani (statements, directives na objectives) iliyoainishwa katika sera fulani. Kwa mfano, sheria ya mazingira ya mwaka 2004 ipo katika kuweza kuhakikisha sera ya mazingira ya mwaka 1997 inatekelezeka na directives zake kuwa enforced. Vivyo hivyo kwa sheria mbalimbali hapa nchini, naelewa utaratibu ndiyo huo. Na mara nyingi, sera zisizokuwa na sheria ndizo zenye matatizo hapa nchini katika utekelezaji wake. Kwa mfano hii nyimbo ya Kilimo Kwanza, kwa jinsi ilivyo sasa hata iweje haiwezi kutekelezeka; mpaka pale patakapotungwa sheria ya ku-enforce yake yaliyoainishwa katika sera hiyo, ndipo sera yaweza kutekelezwa kwa mafanikio. Hivyo sera uandaliwa na kutoa directives na statements za namna gani ya kufanikisha malengo ya sera husika, lakini ili kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa, sheria utungwa kwa ajili ya ku-enforce statements na directives husika (ambapo taratibu uwekwa {kupitia charges, penalties, fines, imprisonment} in-case directives na statements hazitekelezwi kama ilivyoainisha); kisha sheria yaweza kuwa supported na regulations ambazo utoa miongozo na taratibu za ku-enforce sheria husika.
Sasa nikirudi katika suala la Azimio la Arusha, ni vyema
Waberoya umekiri kwamba azimio lilikuwa lina
NIA nzuri. Hata
W. J. Malecela awali alisema kwamba azimio lilikuwa lina mambo mazuri ya kusoma, pengine yasiyotekelezeka, vyema pia. Sasa kama nyote mmeweza kukiri
NIA nzuri ya azimio, na mmesema wazi kwamba lilikuwa halina meno ya kulitekeleza, kwani sheria pekee ndiyo inaweza kufanya hivyo, je, hamwoni ni wasaa muafaka wa kuwa na mjadala wa namna gani tunaweza kutumia misingi mizuri ya azimio (iliyo relevant na today's context) katika kuweza kuandaa na kutunga sheria ambazo zitaweza - by default - kupelekea utekelezaji wa azimio?!
Tunaweza kutumia misingi ya azimio (kama masuala la kupinga unyonyaji, uwajibikaji wa viongozi na watumishi wa umma {kupitia miiko ya uongozi}, kujitegemea na suala la siasa na uongozi bora) katika kuandaa na kutunga sheria zitakazo enforce masuala hayo. Sheria itakayoweka bayana nini kitafanyika endapo kiongozi/mtumishi wa umma akienda kiyume na miiko husika, taratibu a, b, c, n.k. zitachukuliwa dhidi yake; sheria itakayoweka bayana namna ya kuiwajibisha serikali inayoshindwa kukusanya kodi kwa ajili ya maendeleo ya dola na taifa nzima - kwa vile suala la kujitegemea katika azimio lilijikita katika kupanua uwigo wa ukusanyaji wa kodi, sasa tunaona serikali inavyoshindwa kila wakati kuongeza uwigo wa mapato kupitia kodi - huku ikitoa msamaha mkubwa sana wa kodi. Sasa kwa msingi huo, azimio linatupa msingi mzuri wa kuandaa sheria itakayoweza kutoa taratibu za nini cha kufanya endapo serikali itashindwa kukusanya kodi kwa ajili ya kulifanya dola lisiwe tegemezi.
Naamini nia yetu sote ni kuona taifa letu linasonga mbele pamoja na watu wake- sio linasonga mbele na viongozi wake tu. Sasa ndugu Waberoya na Willie, tukiuweka mjadala katika misingi hiyo, ninaamini tunaweza pata hitimisho litakalokuwa na manufaa kwa taifa letu kwa ujumla. Otherwise, mjadala ukiendelea kama ulivyo, hakika hatuwezi kufika mwisho - tutabaki katika kuponda na kupinga azimio bila ya kuleta wayforward (hapa msije na azimio lenu la Zanzibar a.k.a ubepari uchwara - kwani hadi sasa hamjaonyesha mafanikio yake halisi).