Cicadulina
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 977
- 2,370
Masaa 2 yaliyopita mfungaji bora wa ligi kuu msimu wa 2023/2024 na mchezaji bora namba 2 Stephan Aziz Ki ametumia ukurasa wake rasmi wa Instagram kuwaaga mashabiki, wanachama, viongozi, wachezaji wenzie na Rais wa Yanga na kuwatakia kheir.
Ilikuwa ngumu kama ambavyo Bin Kazumari aliripoti awali kwamba kutoa dola za kimarekani 500,000/ (1.3bn) kwa mkataba wa miaka 2 na mshahara wa dola 20,000/ (54M) kwa mwezi ilikuwa ngumu sana kwa Yanga ambayo msimu ujao wanaweza kuhitaji saini ya PACOME, YAOYAO, Max, ambao wanamaliza mikataba yao pia.
Shariti gumu pia ilikuwa ni kupata walau dola za kimarekani 250,000/ up front wakati anasaini mkataba.
Wakati huo huo vyanzo mbalimbali vinaripoti kwamba Simba SC wanahusishwa na kuhitaji huduma ya kiungo huyo mchezesha timu na MVP namba 2 wa NBCPL na wao wamemuahidi kumpa mshahara wa dola 20,000 alizotaka na dola 200,000/ kama malipo ya awali (up front payment) huku Yanga wao waliishia mshahara wa dola 15,000 na “makubaliano maalumu” ya malipo ya mafungu, ambayo wapasha habari wanasema mwanadinga huyo kutoka Burkina Faso na wakala wake hawakuwa tayari kwa mpango huo.
Kama kweli wacha tuone nini kinafunguliwa na andiko hili la Aziz Ki kuaga. Yanga watakubali aondoke licha ya ahadi ya Rais wao kwamba wachezaji muhimu wote HAWATAONDOKA klabuni hapo? Kweli atajiunga na Mnyama?
BIN KAZUMARI MTIPA (The voice of the voiceless)