Aziz Ki alivyompoteza SAKHO kwenye magoli ya CAF Confederation Cup

Watu hapa badala ya kumuelimisha mleta uzi tofauti kati ya goli bora la msimu na mfungaji bora wa msimu wao wanamdhihaki. Ngoja mimi nijaribu kumwelimisha mleta uzi.

1. Mfungaji bora wa msimu. Huyu ni yule mchezaji aliyefunga idadi kubwa ya mabao ktika msimu mzima wa mashindano kuwazidi wachezaji wenziwe wote. Hapa mara nyingi kuna kuwa hakuna kupiga kura kumchagua mshindi bali mshindi hutokana na kuhesabu tu nani ana magoli mengi.

2. Goli bora la msimu ni lile goli linalofungwa katika hali isiyo ya kawaida na zaidi sana katika hali ya ufundi na kufuraisha watazamaji. Hapa huteuliwa baadhi ya magoli halafu watu hupewa nafasi ya kupigia kura goli mojawapo kati ya magoli kadhaa yaliyochaguliwa. Kikubwa vigezo na masharti kutoka kwa waandaaji wa tuzo husika huzingatiwa.

Kwa hiyo Sakho japo ana magoli machache lakini yupo Morocco na Babra kwenye tunzo sasa hivi kwa sababu mojawapo kati ya hayo magoli yake machache lile lgoli lake tamu la "bicycle kick" limeingia fainali kati ya magoli matatu bora kabisa.

Ni mtizamo wangu kuwa mleta uzi utakuwa sasa umeelewa kwa kiasi fulani tofauti kati ya mfungaji bora na mfungaji wa goli bora la mashindano.
 
Mbwiga Omera aibu yako hii
 
Mkuu umefafanua vizuri ila ni kama umempigia mbuzi gitaa,huyo jamaa siyo mtu wa mpira yeye ni mbobevu wa kunywa uji tu.
 
Kama imeingia na kuuma ichomoe Mkuu..
 
Yanga tunaenda kushitaki CAS haipendezi na haiwezekani aziza kinabo amfunike SAKHO kwa magoli bora matatu halafu asiwepo kwenye list. Hatukubali kabisa. Tunaenda fifa.
Mtaumia sana na Aziz Ki Mwaka huu
 
hivi kumbe JF kuna watu wenye miandiko hii
 
Wewe si ni Manara wewe? Ngoja tukuchomee na huku upigwe ban unatakiwa muda huu uwe kwenye kiduka cha mkeo kule temeke unasaidia kuuza rangi za kucha sasa shupaza tu shingo humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…