Aziz Ki ni Mwananchi Yanga SC kwa mara nyingine tena. Nyumbani kumezidi kunoga sana

Aziz Ki ni Mwananchi Yanga SC kwa mara nyingine tena. Nyumbani kumezidi kunoga sana

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kiungo mshambuliaji wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki, amerejea tena katika Klabu ya Yanga SC baada ya kuacha alama kubwa katika kipindi chake cha awali ndani ya timu hiyo.

Aziz Ki aliitumikia Yanga SC kwa misimu miwili, akifanikiwa kutwaa tuzo mbalimbali ikiwemo Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kiungo Bora na Mchezaji Bora wa Msimu (MVP) kutokana na kiwango chake bora uwanjani.

Mchezaji huyo alikumbukwa kwa uwezo wake wa kufunga mabao muhimu, kutengeneza nafasi za magoli na kuwa mhimili mkubwa katika mafanikio ya Yanga kwenye mashindano ya ndani na kimataifa.

Screenshot 2026-08-15 204621.png
 
Mwenzake Mayele analipwa Mshahara wa Tshs milioni 340 kwa mwezi. Yeye atalipwa Tshs milioni 60 kwa mwezi. Huku wapinzani wake kwa pitch ni akina Doumbia na Ismail Mgunda. Hakuna challenge kabisa hapo.
Unamlaumu yeye kulipwa Tanzania Tsh 60m wakati wewe ni pension yako hiyo ikiongezwa mara mbili kuipata utaandika nyuzi hapa balaa..
 
Mwenzake Mayele analipwa Mshahara wa Tshs milioni 340 kwa mwezi. Yeye atalipwa Tshs milioni 60 kwa mwezi. Huku wapinzani wake kwa pitch ni akina Doumbia na Ismail Mgunda. Hakuna challenge kabisa hapo.
Mjomba, mshahara wako kwa mwezi ni milioni ngapi hadi ufikie hatua ya kumponda mchezaji anayelipwa milioni 60?
 
Mwenzake Mayele analipwa Mshahara wa Tshs milioni 340 kwa mwezi. Yeye atalipwa Tshs milioni 60 kwa mwezi. Huku wapinzani wake kwa pitch ni akina Doumbia na Ismail Mgunda. Hakuna challenge kabisa hapo.
Inategemea nchi na nchi anaweza lipwa hata bilioni moja mwingine akalupwa milioni 100 tofauti za nchi na wa milion 100 akawa na maendeleo makubwa 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom