Aziz P. Mlima.. Almost ambassador?


Sijakupata mkuu.nieleweshe tena tafadhali.
 
Mzee Mwanakijiji,

Ilikuwaje kwa Tanzania ambayo haina dual citizenship mtu ambaye sio raia akateuliwa kuwa balozi? Nasema hivyo kwa maana mtu ukiomba uraia wa nchi nyingine automatically unakuwa umepoteza uraia wa Tanzania.

Binafsi namfahamu Dr. Mlima na tumewahi kutofautiana na pia kukubaliana kwa mengi. Angepata hiyo kazi, angekuwa nafuu mno kuliko wengi wa hao mabalozi wetu.

Kama walimfikiria kuwa balozi, nina uhakika anaweza kufaa kwa kazi mbalimbali pale nyumbani hasa upande wa uchumi.
 


Is it possible to be a dual citizen of the United States of America and another country?


Inategemea, Mkuu. Kama alivyosema Julius, inawezekana kabisa ku-limit ofisi ambazo mtu mwenye dual citizenship anaweza kushika. Kama ilivyo Marekani kwa mtu mwenye uraia wa kuapa! Rais wa Marekani ni lazima awe raia wa kuzaliwa. Ndiyo maana wakina Julius wanakazania kuwa Obama aezaliwa Kakamega!

Amandla........
 
...Mie nina swali dogo...Je wateuliwa wa nafasi kama hizi hawafanyiwi background check na vyombo vyetu vya usalama?
 
Mtanzania,
Good to see you again. Nasikia huyu si wa kwanza. Kuna mtu kasema kuna maafisa wengi tu waliotumika kwenye foreign service wana u duo.Tatizo linakuja pale nyumbani kwa kutokuwa makini katika vetting system, au walimwuliza kama amewahi kuchukua uraia wa nchi nyingine na akakana na hence wenyeji wake wakamuumbua. Pale London nasikia tumeshawahi kuwakilishwa na balozi ambaye naye alikuwa ni duo, au aliyewahi kukana uraia wa Tanzania.
 

Unapolana uraia unatakiwa uandike barua ya kuukana, Na huko nyumbani wanatakiwa kutangaza nadhani mara 3 kwamba umekana.

Hapa naona huyu jamaa alighushi nyaraka, kama alitangaza na kukabidhi gamba la kijani nafikiri wasingemteua.
 
Mzee Mwanakijiji,

..wewe umezungumzia uraia wa nchi mbili, sasa mimi kwa makusudi kabisa nikaenda to the extreme kwa mifano ya wahusika ambao hawakuwa raia wa Tanzania kabisa.

..kama alivyopendekeza Julius, iandikwe sheria ya uraia ambayo itazuia wale wenye dual citizenship kushika nafasi fulani fulani ambazo ni too sensitive.

..personally, napendekeza Raisi wetu asiwe na dual citizenship. pendekezo langu halisukumwi na masuala ya loyalty ktk nafasi ya Raisi, bali ni suala la hadhi tu ya nafasi hiyo.
 
Je, tuko tayari rais wetu awe ni raia wa Tanzania na Kenya at the same time? au wa Rwanda na TZ at the same time au nchi nyingine yoyote? Vipi kuhusu Ubunge, Uwaziri, Ukuu wa Jeshi, vyombo vya usalama n.k?

MMK, Jibu ni hapana. Hii ni tafakari nzuri sana.
 
jokaKuu,
Siyo rais tu. Viongozi wote kwenye sensitive positions. Kuna rafiki yangu Mkenya yeye kachukua uraia hapa Marekani. Anasema ofisini ( anafanya kazi serikalini) walimwuliza kama anatumia bado paspoti ya Kenya. Aliposema yes walimwekea namba 2 kwenye faili lake. Alipoulizia wakamwambia kuwa kuna sensitive information ambazo namba 2 hawezi ku-access kwa sababu ingawa ni raia lakini bado ana loyalty kwa nchi alikotoka. He eventually had to give up his Kenyan passport.
 

Hii ndio SABABU nyingine muhimu ya kutufanya tupitishe SHERIA ya Uraia wa Nchi 2 haraka iwezekanavyo. Watanzania wenye uraia wa nchi 2 wapo ila kama ilivyotokea Scandnavia tunashindwa kuwatumia kulitumikia taifa.

Kwa nini hakuukana uraia wa Scandnavia (sijui nchi gani) na kuurudia Utanzania?
 
Unapolana uraia unatakiwa uandike barua ya kuukana, Na huko nyumbani wanatakiwa kutangaza nadhani mara 3 kwamba umekana..

Sio kweli, hautakiwi kutoa talaka kwa uraia wa Tanzania ili upate wa ng'ambo. Hapo umedanganywa kwa kishindo. Nchi za ng'ambo wala hazijali uraia wako wa asili, ukiwa na vigezo wanakupa bila hata swali moja juu ya uraia wako wa asili.
 
Yebo Yebo,
Alipewa nafasi ya kuukana uraia huo akakataa. That is the issue! He wants to have his cake and eat it too. Yaani atumikie Tanzania, afaidike na baadaye anapostaafu anarudi kwao.
 
Jasusi,

Nipo ndugu yangu ila mambo yamekuwa mengi.

Hiyo ni failure kubwa sana katika vetting system yetu. Inajulikana Dr. Mlima amekaa Sweden muda mrefu, ameoa huko kama sikosei na hata alivyochukuliwa kwenda kumsaidia Mkapa alitokea huko. Ningetegemea wangeanzia huko kuchunguza.

Huko mbele hili tatizo litakuwa hata kubwa zaidi maana watanzania wanaoishi na uraia wa nchi mbili kwa kujificha sasa wako wengi sana.

Kwa udhaifu kama huu, sitashangaa kweli mtu asiye raia kisheria akiweza kuchaguliwa kuwa rais.

Waruhusu tu dual citizenship ili kuwaondolea Watanzania tatizo la kuficha na kudanganya.
 
Hapo ndio inapelekea ile pointi ya Joka Kuu kwamba wamefanya makusudi?
Kwanini wamtake aukane uraia,kwani tuna lack watu wengine wenye qualifications zinazokidhi hadi hapo tutakapo pata ufumbuzi wa uraia wa nchi mbili?
Pia hapo unaposema kuna watanzania wenye uraia wa nchi mbili unaweza kufafanua?
Ningeshukuru mkuu kwasababu kama bado hatujapitisha sheria ya uraia wa nchi mbili,ninavyoelewa ukishapata uraia wa nchi nyingine automatically unakuwa umeukana uraia wa Tanzania,is that true ama niko wrong?Jasusi et al,naona pia mmezungumzia kuhusu existence ya hao wenye dual,how is that possible given my question to Yebo Yebo?
 
Sio kweli, hautakiwi kutoa talaka kwa uraia wa Tanzania ili upate wa ng'ambo. Hapo umedanganywa kwa kishindo. Nchi za ng'ambo wala hazijali uraia wako wa asili, ukiwa na vigezo wanakupa bila hata swali moja juu ya uraia wako wa asili.
MgonjwaUkimwi,

Hapo wote wawili wewe na MkamaP mko sahihi. Kuna nchi ili kupata uraia wao lazima wapate makaratasi ya kuonyesha kule kwenu umeukana uraia wako, nafikiri mfano ni kama Poland. Lakini pia nchi zilizo nyingi hawahitaji wewe uukane uraia wa nchi yako ya mwanzo, mfano ni kama UK.
 
inadaiwa yeye ni raia wa huko huko tayari.. sasa nchi inampendekezaje raia wa nchi nyingine kuwa balozi wake?
Lakini itakuwa jambo jema kama tukimuliza Balozi Mombo kuhusu mambo haya au Membe mwenyewe, ila kwani yupo katika Taifa gani??
 
Jmushi1,

Nafikiri ni wanawake tu ambao sio Watanzania na wameolewa na Watanzania wanaruhisiwa kuwa na uraia wa nchi mbili kwa Tanzania. Pia kuna vijana chini ya umri wa miaka 18.

Makundi mengine yeyote, kama wewe una uraia wa nchi nyingine basi kisheria huna uraia wa Tanzania.
 

Naomba nitofautiane na wewe kidogo hapa, nijuavyo mimi mteuliwa ndio wakwanza kuelezwa juu ya posting anayotakiwa kupewa. Dr Azziz alijuwa fika kwamba yeye ni raia wa Sweden alitakiwa aseme hilo hata kabla ya process. Tatizo naloliona hapa ni watanzania kutokuwa wakweli hata pale maslahi ya taifa yanapokuwa at stake, na kufikiri kwamba kiujanja ujanja wanaweza kupindisha ukweli.

Yeye angesema tu kwamba kwa Sweden haitawezekana, labda nchi nyingine. Hivi ukweli unauzwa kwa shilingi ngapi?
 
Sijakupata mkuu.nieleweshe tena tafadhali.

Nilikuwa nina maana kwamba serikali ilitakiwa ijuwe kwamba tayari alikuwa na uraia wa hiyo nchi ya Scandanavia kwasababu wascandnavia wao ndiyo wameikumbusha serikali yetu kuwa mtu waliyemteua ni raia wao na kwahivyo wakashangazwa ni kivipi raia wao aiwakilishe nchi nyingine nchini mwake yeye mwenyewe....Kwa maana nyingine pia,since serikali yetu bado haitambui uraia wa nchi mbili,ina maana tena kuwa raia wa nchi nyingine ameteuliwa kuwa balozi wa nchi yetu kwenye nchi nyingine ambayo imetokea kuwa nchi ya balozi huyo.
Na kwahivyo basi tatizo halikuwa upande wa Scandnavia,bali upande wa serikali yetu,na swali linalobakia ni kama walikuwa wako aware ama la.
Naomba unijulishe kama umeelewa na kama bado nitajaribu tena ama mwenye kuweza ku add atatoa msaada tutani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…