Aziz P. Mlima.. Almost ambassador?

Kwanini tusifuate mtindo wa India ambao Katiba yao inakataza kabisa dual citizenship lakini wakati huo huo wanawatambua wananchi wao walio nje ya nchi?

Kwa nini tuwafuate Wahindi? Kwa nini tusibuni namna yetu wenyewe ya kudili na watu walio na hali hiyo?
 

Shukrani kwa kunifahamisha. Swali bado liko pale pale, huo uraia wa Japan aliupata lini? Wakati akiwa rais wa Peru, kabla ya kuwa rais, au baada ya kutimka. Utata huu unatokana na kuwa ilibidi aombewe uraia na sio yeye mwenyewe kuomba kwa hiyo inaonekana pengine hakuwa nchini Peru au alikuwa chini ya umri wa kuweza kujiombea.
Asante lakini.

Amandla......
 
inadaiwa yeye ni raia wa huko huko tayari.. sasa nchi inampendekezaje raia wa nchi nyingine kuwa balozi wake?
Dr. Mlima kuwa raia wa Sweden sidhani kama ni kikwazo.

Balozi ni mwakilishi tu wa nchi husika na sio lazima awe raia wa hiyo nchi anayowakilisha ndio maana nchi nyingine huwakilishwa na balozi za nchi tofauti. Nakumbuka kama sijakosea, Seycheles inawakilishwa Tanzania na raia wa kiTanzania.

Aziz atakuwa na matatizo yake. Lakini pia nafikiri yeye sio uteuzi mzuri kwani atakuwa kapewa ajira ambayo hajaisomea wala kuwahi kuifanya bali kwa mazingira ya kiushikaji tu na kuwaacha mabalozi wataalam wakilamba vumbi MOFA Dar.
 
Kweli Tanzania ni kitendawili. Hivi kabla hajatakiwa kurudi kuja kumsaidia mkapa long time ago hawakuchunguza kufahamu kama tayari alishakuwa raia wa Sweeden? Hii inatoa dosari kubwa sana kwa wanausalama wa Tz ndani na nje ya nchi, they are too relaxed au ni ugonjwa gani wanao??

Kwa upade wa Dual citizenship, kwa Tz kwa sasa naona bado tunahitaji muda wa kujiandaa kuweka taratibu sawa na sheria ipitishwe kwa makini. Nina wasi wasi kwa sasa kuwa kwa ninavyomfahamu mwanausalama Membe ni lazima kuna a move fulani ambayo anaikingia kifua!!!!!! Kwa taarifa kuna maandalizi kuwa watanzania wa jamii ya Kiasia wanapanga mikakati ya kuchukua nchi hii?? Ni mipango ambayo wamejiandaa nayo since 2006!!! Believe it or not!! Na ni kupitia SSM!!!! Na ninakuambia kuwa kama hawa waasia watakuwa bado wamo ndani ya Tz hakuna namna ambavyo SSM haitaendelea kuchukua madaraka maana huwa wanachangia mno katika maandalizi ya uchaguzi na wakati wa uchaguzi. They are dangeraous!!!! Wafanyabiashara wote hadi nyumba hadi nyumba wanachanga, achilia mbali wale tycoons.

Labda tuweke kuwa Watanzania by indegenous-wazawa ambao kizazi chao cha kwanza hadi cha nane kinaweza kuwa traced in Tanzania, vinginevyo tunataka kukaribisha matatizo zaidi ya tuliyo nayo.

Pole Dr. Azizi P. Milima!!
 
Maane,
Umegusia kitu ambacho nimewahi pia kukisikia. Kuna mtu alinidokeza kuwa hili wazo la dual citizenship lilibuniwa na Rostum Aziz wakati wa utawala wa Mkapa.
Mkapa akamaliza muda wake kabla ya kulifanyia kazi sasa limeibuliwa upya chini ya awamu ya nne na nina hakika baadhi ya Watanzania (wadanganyika) watakuwa wakipiga makofi lakini watakaofaidi matokeo yake ni wengine kabisa. Stay tuned!
 

Aliyekuwa Golikipa wa Yanga Marehemu Sahau Kambi alikuwa balozi wa Commoro Nchini Tanzania.
Marehemu Khalid Alex makondeko naye alikuwa na hadhi ya kibalozi wakati akiwa Mtanzania.
narudi kusema kuwa uraia sio issue kabisa. kuna mengine.
 
Aliyekuwa Golikipa wa Yanga Marehemu Sahau Kambi alikuwa balozi wa Commoro Nchini Tanzania.
Marehemu Khalid Alex makondeko naye alikuwa na hadhi ya kibalozi wakati akiwa Mtanzania.
narudi kusema kuwa uraia sio issue kabisa. kuna mengine.

Sina uhakika lakina mnachosema kama ni honarary ambassadors ambao mara nyingi wanakuwa ni raia wa nchi wanayowakilisha.

Sidhani kama kwenye case hii jamaa yetu alikuwa anapelekwa kama honary ambassador. Nchi husika lazima itoe maoni yake kuhusu mtu anayepelekwa kuwa balozi. Sasa kama Sweden walisema huyo ni raia wao na TZ hatuna dual citizenship, nafikiri hiyo ilikuwa sababu tosha ya jamaa kukosa cheo.

Watu wengine wanataka mpaka hao waliosomea uhusiano wa kimataifa na kufanya kazi foreign. Siku hizi nchi nyingi zinaanza kuteua mabalozi ambao sio lazima wawe kwenye hiyo category.

Mama yetu hapa UK ni mmoja wapo na amefanya kazi nzuri sana kuliko hao waliomtangulia.
 
Waruhusu tu dual citizenship ili kuwaondolea Watanzania tatizo la kuficha na kudanganya.

What a cheap solution......have nothing personal na wewe kaka lakini kama ndio mitizamo hii then wacha tuendelee na POLITICAL MERCINARY wetu kule KYELA.

omarilyas
 
What a cheap solution......have nothing personal na wewe kaka lakini kama ndio mitizamo hii then wacha tuendelee na POLITICAL MERCINARY wetu kule KYELA.

omarilyas
Omarilyas,
Hizi ndio very cheap politics na ambazo hazitujengi hapa JF. Kwasababu unajua nina uhusiano na siasa za Kyela huwezi kujizuia kuweka vijembe?

Hapa tunaelemishana na kwa taarifa mimi naunga mkono dual citizenship hata kama mimi mwenyewe nilipopata nafasi ya kufanya hivyo nilikataa. Binafsi sihitaji passport ya pili ili kufanikisha mambo yangu lakini bahati mbaya sio kila mtu ana bahati kama hiyo. Kuna vijana wengi tu nchi kama UK, tena ambao hawana uhusiano wowote na system huko nyumbani ambao kuwa na passport ya hapa kumewaondolea usumbufu kibao na kuwaongezea nafasi ya kuweza kujitegemea wao na familia zao.

Watanzania ifike mahali tuachane na hizi tabia za kuona jambo halifai mpaka tuwe na personal interests.

Kwasasa kuna Watanzania wengi tu wana passports mbili na wanachofanya ni kujificha ficha. Kama tumeshindwa kuwashughulikia hao ni kwamba tunahangaika na sheria ambayo tumeshindwa kuilinda.

Huyo Dr. Mlima mwenyewe wamejua ana uraia wa nchi nyingine na bado anaendelea kuwa mshauri wa rais Mkapa, hapo tuko serious kweli?
 
Aliyekuwa Golikipa wa Yanga Marehemu Sahau Kambi alikuwa balozi wa Commoro Nchini Tanzania.
Marehemu Khalid Alex makondeko naye alikuwa na hadhi ya kibalozi wakati akiwa Mtanzania.
narudi kusema kuwa uraia sio issue kabisa. kuna mengine.


.....point of correction..

Marehemu sahau kambi hakuwa wala hajawahi kuwa balozi wa nyumba kumi sembuse ubalozi BALI Alikuwa afisa utumishi wa kampuni ya mdogo wake Balozi wa heshima wa COMORO ..ndugu SALEH BALHABOU....aitwae Meley BALHABOU.
 
KWA kuongezea ...nchi yeyote inaweza kumchagua raia wa nchi nyingine kuiwakilisha pale ambapo sababu za kilogistik au kiuchumi zinaikwaza nchi ile kutuma raia wake pale..

pia nchi rafiki zinaweza kushirikiana kuwakilishana pale ambako mwenzake hayupo....mfano kwa nchi zisizokuwa na maslahi sana ..inaweza kuamuliwa na nchi rafiki kama za afrika mashariki ..kuwa mmoja wao aliye na ubalozi pale ...akasimamia maslahi ya wenzake...au pia ikiwa nchi yeyote yenye makubaliano hayo haipo kwa sisis watanzania...ikitokea upo nchi ya aina hiyo basi ...unaweza kwenda kwenye ubalozi wa UINGEREZA na kupata msaada wa awali kama nchi mwanachama wa jumuia ya madola.....
 
kanda2 said:
Aliyekuwa Golikipa wa Yanga Marehemu Sahau Kambi alikuwa balozi wa Commoro Nchini Tanzania.
kanda2 said:
Marehemu Khalid Alex makondeko naye alikuwa na hadhi ya kibalozi wakati akiwa Mtanzania.
narudi kusema kuwa uraia sio issue kabisa. kuna mengine.



kanda2,

..ubalozi unaouzungumzia wewe ni Ubalozi wa Heshima au Honorary Consualar. hawa huwa wanateuliwa kuwakilisha maslahi ya nchi husika ktk eneo ambalo nchi hiyo haina mwakilishi/balozi.

..Dr.Alex Khalid[r.i.p] na Daniel Yona waliwahi kuwa mabalozi wa heshima wa Seychelles na Ghana hapa Tanzania. nadhani hata Uholanzi ambapo hatuna ubalozi kuna Mholanzi ameteuliwa kuwa Honorary Consular wetu.

..sasa huyo Dr.Mlima anaweza kuteuliwa balozi wa heshima huko anakoishi lakini hatakuwa na hadhi na diplomatic staff under his supervision kama mabalozi wa kawaida. pia majukumu yake yatakuwa ni madogo-madogo tu kama kutoa visa, kutangaza utalii, kutangaza biashara, etc etc.
 
What a cheap solution......have nothing personal na wewe kaka lakini kama ndio mitizamo hii then wacha tuendelee na POLITICAL MERCINARY wetu kule KYELA.

omarilyas


Kwa mtu unayeheshimika kama wewe sikutegemea ungekuwa na maoni kama haya.Acha kukatisha tamaa wenzako mkuu.Mtanzania amechangia vizuri sana katika hii thread.Cha ajabu mazuri yote aliyoyachangia hukuyaona,ukaamua ku single out hako ka statement ili umshambulie.
Typical watanzania,mtu akifanikiwa yeye basi ni kuwekea vikwazo na kukatisha tamaa wengine
 

Kwa kawaida mkuu dual citizenship zinakuwa na provisions zinazo elezea "rights & duties". Provision hizo zinaelezea mtu mwenye uraia mbili ana haki ya kupewa nafasi gani za uongozi wa nchi. Usually mtu mwenye dual citizenship hawezi kupewa uraisi au cheo chochote ambacho kipo inline kumrithi raisi. Pia kuna vyeo vingine vinaweza kuainishwa ambazo haruhusiwi kupewa au kugombea.

Personally I believe mtu mwenye uraia wa sehemu mbili kuna nafasi hatakiwi kabisa na hastahili kuwa nacho haswa hizi za kiserikali. Mtu hawezi kuserve two masters na saa nyingine interests zina conflict.
 
inadaiwa yeye ni raia wa huko huko tayari.. sasa nchi inampendekezaje raia wa nchi nyingine kuwa balozi wake?
kwani raia wa nchi nyingine hawezi kuwa balozi kwa nchi nyingine? Nina mifano hapa, enzi za nyuma kidogo Dk Alex Khalid(the late) aliwahi kuwa balozi wa(nafikiri Comoro) nchini Tanzania, vile vile kuna huyu Shamo(Shamo industries) ni mfanyabiashara wa tanzania mwenye asili ya Comoro na ni balozi wa Comoro hapa bongo, Am I right....
 
Hao uliowataja hawakuwa mabalozi kamili. Walikuwa ni honorary.
 

You are wrong.

Amandla.....
 
Kwani Aziz si ni msaidizi wa Mkapa? au nimepitwa na wakati?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…