- Source #1
- View Source #1
Wakuu,
Kwa taarifa nilizokua najua awali ni kuwa mchezaji Azizi Ki alimaliza mkataba wake na timu ya Yanga na kusaini Mkataba na klabu ya Wydad ya Morocco, alafu leo nimekutana na hii eti kasaini mkataba na Azam, naombeni msaada wakuu wa Jamii check
Kwa taarifa nilizokua najua awali ni kuwa mchezaji Azizi Ki alimaliza mkataba wake na timu ya Yanga na kusaini Mkataba na klabu ya Wydad ya Morocco, alafu leo nimekutana na hii eti kasaini mkataba na Azam, naombeni msaada wakuu wa Jamii check
- Tunachokijua
- Stephan Azizi Ki ni mchezaji wa mpira kutoka BurkinaFaso ambaye amaewahi kuchezea klabu mbalimbali ikiwemo ya Yanga kutokea nchini Tanzania na hivi karibuni iliripotiwa kuwa amejiunga na timu ya Wydad Athletic ya nchini Morocco.
Madai
Zipo taarifa zilizosambaa leo Julai 18, 2025 zikieleza kuwa aliyewahi kuwa mchezaji wa Yanga, Stephan Aziz Ki amehamia Azam FC kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Ufuatiliaji uliofanywa umebaini kuwa Azizi Ki bado ni mchezaji wa Wydad Athletic club ya nchi Morroco ambapo alijiunga na timu hiyo akitokea Yanga.
Katika ukurasa wake wa instagram Aziz Ki anajitambulisha kama mchezaji rasmi wa Wydad Athletic club na timu ya taifa ya Burkinafaso. Aidha Julai 17, 2025 Azizi Ki pamoja na Wydad kupitia kurasa zao za mtandao wa Instagram walichapisha picha zinazomuonesha mchezaji huyo akiwa mazoezini.
Kupitia ukurasa wao wa Instagram Azam Football Club hawajamtambulisha mchezaji huyo kama utambulisho wao wa hivi karibuni.
Grafiki zilizotumika kusambaza ujumbe huo pia ni za kughushi na hazijachapishwa na vyanzo hivyo kama inavyoonekana. Aidha pia zina makosa mbalimbali ya ikiwemo ya kiuandishi.